Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatano, 5 Februari 2014

SKAUTI WATOA MSAADA WA HUDUMA KATIKA MAAFA YA MAFURIKO MJINI MOROGORO-DUMILA.

SKAUTI WATOA MSAADA WA HUDUMA KATIKA MAAFA YA MAFURIKO MJINI MOROGORO-DUMILA.


Skauiti washiriki katika kutoa msaada katika maafa ya mafuriko yaliyo tokea mjini morogoro-dumila dhidi ya mvua zilizo nyesha kwa wingi hadi kupelekea mafuriko wilayani humo{dumila}. kufuatia maafa hayo chama cha skauti tanzania kupitia kamishna msaidizi kitengo cha maafa kilipeleka kikosi cha huduma na uokoaji majini na nchikavu ili kushirikiana na vikosi vyengine vya serikali na binafsi katika kutoa msaada unaohitajika.
Kamishna mkuu msaidizi kitengo cha maafa. Alhajj, Juma Massud

Kufuatia tukio hilo skauti pia iliweza kuzaa matunda juu ya jambo kubwa wlilolifanya katika kambi ya dhalura iliyo tengenezwa kufuatia tukio hilo, serikali kupitia mkuu wa mkoa wa morogoro iliikabidhi skauti dhamana ya kuandaa na kuweka maingira ya kambi kwakuwa skauti ni wazoefu juu ya masuala ya kambi.

Skauti wakiwa katika shughuli za ujenzi wa vyoo kwaajili ya kukamilisha zoezi la uaandaji wa eneo la kambi kama walivyo agizwa na mkuu wa mkoa wa morogoro.
Skauti wakiwa katika shughuli za ujenzi wa vyoo kwaajili ya kukamilisha zoezi la uaandaji wa eneo la kambi kama walivyo agizwa na mkuu wa mkoa wa morogoro.

Lakini pia kama Skauti walichukua nafasi hiyo kwa kukitan
gaza chama cha Skauti katika jamii na kusambaza ujumbe wa Amani kupitia vijana wa shule ya sekondari Dumila na wana kijiji kiujumla. pia waliweza kuanzisha kundi la skauti na kulipa mafunzo ya mwongozo kwa kuanzia juu ya skauti na shughuli zake kiujumla.
 Ni wanachama wapya wa skauti ambao walikubali kwa moyo wa dhati kujiunga na chama cha skauti baada ya kuona yale waliofanya skauti katika kusaidia kijiji chao baada ya mafuriko kutokea.
 Vijana wadogo wakiwa pamoja na skauti katika kuashiria upendo wa dhati juu ya walio watendea baada ya maafa yalio wakuta katika kijiji chao-dumila.
 Wana kijiji wakiwa katika picha ya pamoja na skauti baada ya kuwahubiria uskauti na madhumuni yake na kuwaachia ujumbe wa Amani ili waweze kuishi vyema kwa kufuata misingi halisi ya kibinaadamu.
Kiongozi wa kikosi chahuduma na uokoaji{majini} akiwa katika kiashirio cha Ujumbe wa Amani baada ya kuzungumza na wakaazi wa kijiji cha Dumila mjini Morogoro.

Kiongozi wa kikosi cha maafa na uokoaji{majini}, pia ni msimamizi wa vijana katika masuala ya Ujumbe Amani Tanzania {katika ngazi ndogo ya Taifa} akiwa na mmoja kati ya vijana wa kijiji hicho kilicho kumbwa na maafa ya mafuriko.



Mwisho kiongozi huyo aliwataka skauti wote kuwa naa ushirikiano wa pamoja katika kukijenga chama cha skauti katika misingi na maadili yaliyo mema, na kuwa tayari akati wowote kulitumikia taifa pale inapotokea tatizo kama hilo la mafuriko na mengineyo. pia alisisitiza juu ya kundi hilo jipya la skauti kuwa na moyo wa upendo kwa kila mmoja na kpeana ushirikiano na kuishi kutokana na misingi, kanuni na ahadi ya skauti.