Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 3 Julai 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI DUNIANI. THEME ‘‘Right of Peoples to Peace”

SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI DUNIANI

Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ni siku iliyopangwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukomesha vita, kutoa elimu juu ya amani na kuimarisha haki za binadamu ambayo husherehekewa tarehe 21 Septemba ya kila mwaka.

Mwaka huu 2014, Skauti (Tanzania) tutaungana na Mataifa mengine ya Dunia katika kusherehekea siku hii muhimu ikiwa imebeba kaulimbiu isemayo, ‘‘Right of Peoples to Peace” 

Lets meet to the summit of Mt. Kilimanjaro with the Peace message.

Mh. Abdulkarim Shah (Mb) Kamishna mkuu
 Chama Cha Skauti Tanzania.
Hivyo Ndugu, Skauti, kwa waraka huu tunaombwa kutangaza kauli mbiu hii kwa njia mbambali zitakazoweza kukuza Amani katika nchi yetu ya Tanzania na Dunia kwa ujumla.


                                                       
  







   Utaratibu wa Upandaji Mlima:



                                                                Umri:



> Skauti watakaoruhusiwa kupanda Mlima Kilimanjaro ni wale walio na umri wa miaka 12 na kuendelea, wavulana, wasichana na viongozi wao.

                                                                 Afya:

> Kila mshiriki atahitajika kupima afya yake katika kituo chochote cha afya kujihakikishia kuwa na afya bora kabla ya kupanda mlima.
                                       

                                                         Vifaa vya Kubeba


> Vifaa vya usafi:- Sabuni ya kuogea, sabuni ya kufulia, mswaki, dawa ya mswaki, mafuta ya mgando n.k.
> Mavazi:- Nguo nzito za baridi Masweta, jackets, nguo za michezo, soksi za mikono na miguu, kofia za baridi n.k.

                                                           Ada ya Ushiriki:


> Kila mshiriki atawajibika kuchangia kiasi cha Tshs. 150,000/=  ambayo itajumuisha gharama za kuingia mlimani, gharama za kupanda mlima, chakula na malazi kwa kipindi chote cha siku za kupanda mlima.
> Gharama nyingine za usafiri kutoka na kurudi katika mikoa husika na ada za kutoka nje ya mikoa zitagharamiwa na mshiriki mwenyewe binafsi.
> Malipo ya kila mshiriki yanahitajika kulipwa kupitia Akaunti ya Chama cha Skauti Tanzania, iliyoko katika Benki ya National Bank of Commerce (NBC) tawi la Samora,
Account Number 012103010625. Baada ya malipo, Makamishna wa Mikoa watawajibika kutuma majina ya Skauti watakaolipa na namba za stakabadhi za malipo ya Bank Makao Makuu ya Chama kwa uthibitisho.
                                                         

                                                            Kuthibitisha Ushiriki:

> Washiriki watahitajika kuthibitisha ushiriki wa kupanda Mlima kwa Kujaza fomu na kuirejesha Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania kwa njia ya barua pepe (Email) kabla ya tarehe 18 Julai 2014 au kupitia kwa Makamishna wa Mikoa.

                                                                     RATIBA:


S/No.          TAREHE                                   TUKIO                                       MUHUSIKA                 
1.          16 - 17 Septemba 2014        Kuwasili Mkoani Kilimanjaro    Uongozi wa Skauti Mkoa wa
                                                                                                                Kilimanjaro na Uongozi wa                                                                                                            Skauti\ Makao Makuu.
                                                                                                                                                                
  2.        18 - 21 Septemba 2014        Kuwasili Kileleni mwa Mlima           Skauti wapanda Mlima
                                                           Kilimanjaro                                                                       
  3.        22 Septemba 2014                Kurejea chini ya mlima Skauti         wapanda Mlima              
  4.        23 Septemba 2014                Kuondoka Kilimanjaro                   Skauti wote                     

Ni mategemeo yetu kuwa Skauti tutajitokeza kwa wingi kuonyesha mshikamano wetu katika kupeleka ujumbe wa Amani kwa njia kupanda mlima wetu Kilimanjaro, Mlima mrefu Barani Afrika wenye kuleta Amani, Upendo na Matumaini pale ambapo hakuna matumaini

Kwa maelezo zaidi kuhusu upandaji mlima, na watakao hitaji fomu za ushiriki {kwenda kusherekea siku ya Amani duniani} tafadhali tutumie ombi hilo la kupata fomu hiyo kupitia :

Mobile: +255 713 295 715
Tell: +255 2222 153342
Fax: +255 2222 1248 807
Email: Tanzani Scout Association



MLIMA KILIMANJARO








Alhajj. Omar Khatib Mavura Mratibu Messengers
of Peace Taifa.



















Murtadhwa Rashid Abdallah Mratibu Messengers
of Peace Mkoa (Dar-es-salaam)



















https://www.facebook.com/pages/Messengers-of-Peace-Tanzania-MOPTZ/1408726232704353?ref_type=bookmark

HATIMAE JUKWAA LA VIJANA LAPATA WAJUMBE WA KAMTI KUU TANZANIA. {TANZANIA YOUTH COMMITTEE} 2014-2016

JUKWAA LA VIJANA TANZANIA, {TANZANIA YOUTH FORUM} 28-30 JUNE,2013 BAHATI CAMP-MOROGORO.


          Chama cha Skauti Tanzania chapata uongozi mpya wa jukwaa la vijana "Youth Forum" yenye wajumbe sita (6) chini ya mwenyekiti Bw. Chacha N. Mwita ambae amekabithiwa rasmi jukumu hilo mapema wiki hii baada ya kuchaguliwa na na vijana walioshiriki jukwaa hilo kutoka mikoa tofauti iliyopo nchini Tanzania, uchaguzi huo uliofanyika 28-30 june, 2014 sambamba na kuendeshwa kwa kongamano hilo juu ya maendeleo ya uskauti na vijana wa skauti kiujumla.


Timu iliyoshiriki jukwaa la vijana 


        















         

         Aidha nae Bw. Chacha (baada ya kuchaguliwa kwa nafasi hiyo) aliitaka kamati yake kuwa makini na kuwa tayari kukitumikia chama cha Skauti Tanzania (kwa kutumia nyadhifa walizo nazo kama viongozi wa vijana nchini) kwa hali na mali ili kuhakikisha wanafikia malengo na dhamira ya chama cha Skauti kidunia.
         Pia Bw. Chacha (Mwenyekiti) alitoa wito kwa vijana wa skauti nchini (Tanzania) kuonesha na kuwapa ushirikiano wanakamti hiyo ya jukwaa la vijana la Tanzania iliyoundwa 30 june, 2014  ili kufanikisha utendaji wa kamati hiyo.

       
         Vile vile Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani) alisisitiza juu ya ushirikiano wa vijana (skauti) na kamati hiyo ili kuleta manufaa kwa wana chama (skauti) katika nche yetu na ulimwengu kiujumla. 
          Ndugu katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani Bw. Murtadhwa R. Abdallah aliwaeleza kwa upana zaidi wajumbe walio hudhuria kongamano hilo juu ya masuala ya ujumbe na wajumbe wa amani (Semina fupi elekezi) na kuwataka wajumbe hao waliohudhuria kongamano hilo kuwa wajumbe (mabalozi) wa kulifikisha na kulifanyia kazi suala la ujumbe na wajumbe wa amani katika mikoa yao na kuanza kulifanyia kazi kwa vitendo suala hilo.
Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani)
Sambamba na viongozi hao wa jukwaa la vijana, pia Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini) aliipa baraka kamati hiyo ya jukwaa la vijana nchini na kuwapa wosia wa kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufuata misingi na kanuni za skauti. 
Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini)

        Pia alimalizia kwa kusema kuwa "Jukwaa la vijana ni moja ya chombo kinacho tumiwa katika kufanikisha shughuli za chama, hivyo ni vyema vijana kukitumia chombo hicho katika kuleta mafanikio ndani ya chama..



Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini)akitoa somo kwa vijana waliohudhuria jukwaa hilo.



UONGOZI WA KAMATI YA JUKWAA LA VIJANA TANZANIA 2014-2016




Ndugu, CHACHA MWITA 
(Korogwe)
MWENYEKITI

Bi, ANNA EMMANUEL 
(Dodoma)
NAIBU MWENYEKITI
Ndugu, MURTADHWA RASHID
 (Dar Es Salaam)
KATIBU








Ndugu,TITO JACKSON
(DarEs Salaam)
MJUMBE
Ndugu, ALLEN MPANDE
 (Morogor)
MJUMBE
Ndugu, ELAM MOSSES
 (Mbeya )

MTUNZA HAZINA