Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumapili, 25 Desemba 2016

Happy Christmass and Prosperous New year 2017.

The Tanzania Scouts Association Wishes all Scouts, Non Scouts and Supportes a Happy Christmass and Prosperous New year 2017.






We thank you and we are proud of you, we look forward to continue working with you in 2017 and beyound.







This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania


Alhamisi, 8 Desemba 2016

SKAUTI WAPATA MAFUNZO YA MAWASILIANO, TEKNOLOJIA NA HABARI.














Na Rehema Ramadhani


Dar es salaam; Chama cha Skauti Tanzania kwa kushirikiana na chama cha Skauti Poland kimepata mafunzo maalum ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari maarufu kama PR-Lab  kwa baadhi ya wanachama, mafunzo hayo yalichukua takribani siku sita yalianza 27/11 hadi 2/12/2016 katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park kilichopo Mnazi Mmoja jiji Dar es salaam.

Akizungumza na wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania, Mratibu wa  mafunzo hayo Bi.Victoria  Drodz  kutoka Chama cha Skauti cha Poland, amesema wanafarijika kutoa elimu hiyo kwa maskauti wa Tanzania kwani Skauti ni ndugu na tunapaswa kupeana  yaliyo mazuri ili kujenga Skauti kwa pamoja.
“sisi Skauti kutoka Poland tunajiskia vizuri kuungana na kutoa elimu hii ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.  kwa Skauti wenzetu wa Tanzania kwani Skauti hubadilishana mafunzo na ujuzi wa aina mbalimbali  kwa ajili ya kuijenga dunia zaidi ya tulivyoikuta” Alisema Bi.Victoria. 

Tumezungumza na baadhi ya wanachama wa Chama cha Skauti  Tanzania walio hudhuria mafunzo hayo na jinsi  walivyo yapokea.
‘Tumefurahi sana kwa elimu tulioipata kutoka kwa Skauti wenzetu wa  Poland kwani elimu hii hutolewa Vyuo Vikuu au kwa kulipia ili kupata elimu hii, lakini skauti wenzetu  kutoka Poland wametupa elimu hii bure  kwa ajili ya kuijenga Skauti na Dunia kwa ujumla” Alisema mmoja wa wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania.
Tuli zungumza na Mgeni Rasmi aliyekuja kufunga mafunzo hayo Balozi Mstaafu Nicholas Kuhanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendani ya Chama cha Skauti Tanzania alisema, amefarijika  kuona vijana wake wakipewa elimu yenye viwango vya juu na anaamini kupitia vijana hao wachache waliopata elimu hiyo wataisambaza zaidi kwa Skauti wenzao na kwa vijana wote kwa ujumla. 

“Tunafarijika kuona Skauti ya Tanzania inazidi kusonga mbele na vijana wanazidi kupata elimu, hivyo kupitia vijana hawa  wachache waliopata mafunzo haya tuna imani  vijana wengine wataweza kupata  elimu hii pia tuna wakaribisha  skauti wote na kwa wale wasio kuwa Skauti katika maadhimisho ya  miaka 100 ya uskauti Tanzania ifikapo tarehe 28  Juni 2017 mkoani Arusha” Alisema  Balozi kuhanga


Balozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Skauti Tanzania ndugu Nicholas Kuhanga akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Chama cha Skauti cha Poland na Tanzania. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete kilichopo Mnazi Mmoja D’salaam. 

Picha Na Mutadhwa Elbahsan






























This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania