Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 27 Februari 2017

Skauti yazindua Mradi wa “U-Report” kwa ushirikiano na UNICEF

Chama cha Skauti Tanzania, kimezindua programu mpya iitwayo “U-Report”, mradi huu ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNICEF ambapo upo katika nchi nyingi za Bara la Afrika ata Ulaya.

Viongozi wakionyesha bango lenye namba ambayo inatumika kwa kujiunga na “U-Report” katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika tarehe 25/02/2017, wa pili kutoka kulia ni Abdulkarim Shah (Kamishna Mkuu wa Skauti) akifuatiwa na Omary Mkali (mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia) wa pili kutoka kushoto ni Rashid Kassim Mchatta (Naibu Kamishna Mkuu, aliyevaa fulana nyeupe), Emmanuel Bayo (mwakilishi kutoka UNICEF, aliyevaa fulana nyeusi) Wa kwanza kulia ni Joackim Assenga (Kamishna wa Skauti Wilaya ya Temeke) na wa kwanza kushoto ni Omary Mavula (Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Skauti Programu ya Vijana)

Chama cha Skauti Tanzania, kimezindua programu mpya iitwayo “U-Report”, mradi huu ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNICEF ambapo upo katika nchi nyingi za Bara la Afrika ata Ulaya, mradi wa “U-Report” umezinduliwa wakati wa maadhimisho ya wiki ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa skauti duniani “Founders day” katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Tanzania, Upanga, Dar es Salaam, tarehe 25 Februari 2017.

U-Report ni programu maalum kwaajili ya kuripoti matukio mbali mbali yanayotokea kwenye jamii zetu kama vile unyanyasaji wa watoto/kijinsia, matukio ya uhalifu, ajira za utotoni, ukatili dhidi ya watoto.
Aidha, imetolewa rai ya kujiunga kwa kutuma sms yenye neno “Sajili” kwenda namba “15070” sms zote ni Bure (bila ya kutozwa gharama yoyote), huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa mitandao ya simu ya kiganjani ya Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel aidha mradi huo unatarajia kujiunga na mitandao mingine ya simu ya kiganjani ya Halotel pamoja na TTCL.

Katika uzinduzi huo ulioambatana na kuazimisha wiki ya kumkumbuka mwanzilishi wa Skauti duniani Robert Baden-Powell (a.k.a BP) aliyezaliwa tarehe 22 Februari 1857. Ambapo kwa Tanzania Bara uliingia mwaka 1917, takribani Skauti zaidi ya 5000 waliudhuria kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi kutoka mkoa wa Pwani.

Habari na Murtadhwa El bahsan
Picha na PR Lab (TSA)



















Rais Mstaafu Mzee Mwinyi Aongoza Matembezi ya Skauti Dar

RAIS mstaafu ambaye pia ni Mdhamini wa Skauti Tanzania, Mzee  Ali Hassan Mwinyi,  Jumamosi (tarehe 18 Februari 2017) ameongoza matembezi ya hisani (Charity Walk) kwa ajili ya kuchangisha fedha  za kufanikisha shughuli za Chama cha Skauti Tanzania  kutoka kwa wadau na marafiki wa skauti kuelekea maadhimisho ya siku ya Skauti Afrika na miaka 100 ya Skauti Tanzania matukio yote mawili yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Arusha.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) alipokua akiongoza matembezi ya hisani kutokea makao makuu ya skauti upanga kuelea viwanja vya Bwalo la Polisi, Oyster Bay jijini Dar, kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako aliyeungana naye.

Matembezi hayo ya hisani yameanzia katika kiwanja cha Skauti kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam na kuishia katika bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officers Mess) la Oysterbay kuanzia saa 12 asubuhi na kufikia tamati majira ya saa nne asubuhi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa matembezi hayo, Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza,  alisema kuwa chama hicho kinatarajiwa kusherehekea Siku ya Skauti Afrika na kuadhimisha miaka 100 tangu Skauti kuingia Tanzania Bara (Tanganyika).  Chama hicho hapa nchini kilianza mwaka 1917 na mwaka huu wa 2017 kinatimiza miaka 100.
Uchangishaji mwingine wa fedha kwa njia ya chakula (Dinner Gala Fund Raising) unategemea kufanyika Februari 24  katika Hoteli ya Serena ya ijini Dar es Salaam.

Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza, akizungumza jambo baada ya kuhitimisha matembezi.

Kwa upande wake kamishna Mkuu wa Skauti Abdulkarimu Shah amesema bado wanaendelea kuwahamasisha vijana kujiunga katika chama hicho ili kuwa waadilifu, wajasiri, wabunifu na wenye maarifa ili kufanikiwa na kuepukana na magonjwa yanayoepukika ikiwemo Ukimwi.
Maadhimisho hayo yatafanyika juni 24 hadi julai mosi mwaka huu mjini Arusha, yenye kauli mbiu inayosema “kuwajenga wazalendo na kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya nchi”.
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Abdulkarim Shaha, akizungumza jambo baada ya kuhitimisha matembezi.

Aidha, Rais Mstaafu ALI HASSAN MWINYI, amezindua mfuko wa kuchangia maandalizi ya mkutano wa Skauti wa Afrika, uanaotarajiwa kufanyika Arusha, Machi mwaka huu ambapo ameonyesha kufadhaishwa na baadhi ya wazazi wanaoshindwa kuwalea watoto wao katika roho na kweli hivyo kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa maadili na kihalifu ikiwemo matumizi ya vileo na dawa za kulevya.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa zaidi ya watu 5,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya bara hilo wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa maskauti kuanzia Mach 8 mpaka 11 mwaka huu Mkoani Arusha, ikiwa ni maadhimisho ya kila mwaka ya siku ya skauti Afrika yanayokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 1OO ya skauti Tanzania.

Mzee Mwinyi, ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa skauti Tanzania, mwenye umri wa miaka 93 sasa, akiwa bado ni mkakamavu na mwenye siha njema, alitembea kilometa 6.5 kutoka Makao makuu ya skauti Upanga mpaka viwanja vya bwalo la maafisa Polisi Ostabei, katika matembezi ya hisani kuchangia maandalizi ya mkutano huo unaotarajiwa kugharimu shilingi milioni 800.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa JOYCE NDALICHAKO, ambaye kwa mujibu wa katiba ya skauti ni Rais wa skauti kutokana na madaraka yake, amewasihi wazazi kuwapeleka watoto wao skauti wakajifunze maarifa, stadi za maisha na uzalendo, badala ya kuwaacha kama mifugo isiyo na mchungaji na katika hatua nyingine, amewaonya walimu wote amabo shule zao zitabainika kuwa vijiwe vya wanafunzi kujifunzia mambo yasiyofaa, serikali haitawavumilia.
Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza jambo baada ya kuhitimisha matembezi.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) alipofika katika viwanja vya Bwalo la Polisi, Oyster Bay jijini Dar, wakati alipohitimisha matembezi ya hisani. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako aliyeungana naye.









Habari na Sasi
Picha na Murtadhwa Elbahsan

Jumamosi, 11 Februari 2017

Tanzania Scouts Charity Walk 18-02-2017

 

Chama cha Skauti Tanzania Tunawakaribisha skauti wote, wazazi na rafiki wa skauti wote kwenye matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufankisha Maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika na Miaka 100 ya Skauti Tanzania yatakayo fanyika tarehe 18/02/2017 jijini DSM.
Matembezi yataanzia makao makuu ya skauti Upanga, muda wa kuripoti ni saa 12.00 asubuhi na kumalizikia Police Officers Mess Oysterbay 6.00 mchana.

Mgeni rasmi ni Mh. Ally Hassan Mwinyi Rais Mstaafu na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania.
Kiwango cha ushiriki ni kuanzia 15,000/ na kuendelea. Fomu za kuchangia zinapatikana skauti makao makuu.

Ungana nasi kwa kijaza fomu mtandaoni kupitia link hii hapa chini....
https://tanzaniascout.org/2017/02/01/charity-walk/

Mawasiliano.
info@tanzaniascout.org / tscouts2092@gmail. Com
Www.tanzaniascout.org

#nimatembeziyetu