Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 30 Machi 2017

Jukwaa la Wahariri Latoa Tathmini ya wiki moja ya Kususia Habari za Makonda

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.


Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.


Aidha, Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.


Wakati huo huo, kituo cha Clouds kimepongezwa kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.

Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.


Theophil Makunga,

Mwenyekiti TEF

Imetolewa Leo,

Machi 30, 2017

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL-NAJEM NCHINI ATEMBELEA MAKAO YA TAIFA YA WATOTO YATIMA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAAM

Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na watumishi,watoto yatima katika 
Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali jijini 
Dar es Salaaam. 













   





Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa kwenye viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
 

 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akipanda mti katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.

 














 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi bengu za mbogamboga, Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii,Siman Panga
 
Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii, Simon Panga akizungumza katika hafla ya kutembelea miradi mbalimbali katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaaam.

 

Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akiwakatika picha ya pamoja katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.

  
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
 









 




Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia)akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.ambapo alishukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa msaada wa miradi mbalimbali na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora
 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikagua mradi wa maji Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MAKAMU WA RAIS WA KLABU YA SIMBA, GEOFREY NYANGE KABURU AZINDUA TAWI LA SIMBA LA KICHWABUTA BUKOBA

Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu jana amefungua Tawi la kwanza la  Simba mjini Bukoba na kuweza kuwaunganisha Wana Simba wa hapa Kagera. 
Pia katika Uzinduzi huo wa Tawi ambalo lipo Kashabo pia walikuwepo Wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Jonas Gerald Mkude, Kichuya na Wengine. Piacha na Faustine Ruta, Bukoba
 
 

 

 


 

 
Pia wameweza kumshukuru ndugu Omary Makoye, Mratibu wa Tawi wa Klabu ya Simba kwa kuwatembelea wakiwa katika Mchakato wa kuunda Tawi hilo. 

Na pia wameshukuru kwa msaada aliowapa na ulikuwa ukihitajika kwa muda huo. Shukrani pia kwa Ndugu Sued Mkwambi kwa kukubali kuwa mlezi wao wa Tawi.

 

 

 
Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburuakiteta na Wanatawi na wanakagera waliokuwa eneo la Tawi hilo la Kichwabuta.

 


Mh. Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na  Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa leo hii mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba.


 Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu.

 Tawi linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.

Wadau na Wapenzi wa Simba wakiwa tayari kwa Uzinduzi wa Tawi hilo.

  

  
Wakifuatilia kwa karibu Uzinduzi wa Tawi

  
Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu akisaini kwenye Kitabu

MPANGO AFUNGUA WARSHA YA MAENDELEO YA VIWANDA ILIYOANDALIWA NA REPOA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya umuhimu wa taasisi katika Maendeeo ya Viwanda nchini kwa watafiti iliyoandaliwa na taasisi ya REPOA

 Mkurugenzi mkuu wa REPOA Tanzania, Dr Donald Mmari akizungumza juu ya taasisi hiyo na mudhui ya mkutano kwa watafiti

 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakifuatilia kwa makini

 Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa katika mkutano huo

 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo

 Kiongozi wa umoja wa Ulaya  Roeland Van De Geer akizungumza wakati wa mkutano huo

 Profesa Lant Pritchett  kutoka chuo kikuu cha Havard Marekani akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Warsha hiyo Prof Lant ni mmoja wa watoa mada wakuu waliofika katika mkutano huo

 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakisikiliza mada kutoka kwa Prof Lant

Waziri wa Fedha na Mipango , Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki

SIASA Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Atoa Msaada wa Chakula Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Kaseko ametembelea Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema na kutoa Msaada wa Chakula kwa Wagonjwa wenye hali ngumu ya Maisha & Wanaohitaji msaada kutoka kwa wasamalia wema. 

Akikabidhi msaada  huo kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo  Sr. Mariojose kwa niaba ya Wagonjwa wamama na watoto Ndugu Kaseko ametoa Chakula Mahindi Kilo 100, Maharage Kilo 50, Soya Kilo 50, Sukari Kilo 25, Mafuta ya Kupikia Ndoo moja ya lita 20, Sabuni & Juice Vyenye thamani ya Tsh. 700,000/

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha amesema yeye ni mzawa wa Sengerema na amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo wakati wote wa utoto wake hivyo anazifahamu sawia changamoto zinazoikabili huduma ya afya hospitalini hapo na kwamba ameguswa sana Matatizo hayo hivyo na kuamua kuunga Mkono Juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania katika sekta ya Afya.

 Ndugu Kaseko ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbaliwa maendeleo kuisaidia Serikali kuwaletea maendeleo wananchi kwani Serikali ina mambo mengi hivyo peke yake haiwezi ni lazima watu wenye moyo wa kujitolea na wanaopenda maendeleo wajitoe kuisaidia Serikali inaayoongozwa na Rais Magufuli ambayo ukweli inajikita haswaa kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.

 Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo teule ya Wilayaya Sengerema Sr.Mariojose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo na kusema ni wachache sana wenye moyo huo na kumuomba aendelee na moyo huo huo wa kujitolea wa kuwasaidia wenye Shida hasa Masikini.

 Katika hatua nyingine Ndugu Kaseko amekabidhi Madawati Kumi na Tano  manne  ( 4 ) Katika Shule ya Msingi Ibondo Wilayani Sengerema. Ndugu Kaseko ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha amesema anaunga mkono Juhudi za Serikali ya Hawamu ya Tano Chini ya Rais Magufuli na Kwamba Elimu bure imekuja na changamoto kedekede kote nchini na kwamba  serikali inastahili kusaidiwa ili kuhakikisha Elimu bora inatolewa. Ndugu Kaseko ametaja baadhi ya Changamoto hizo ni Uchache wa  Madarasa ya kusomea, Maabara, Madawati, Vyoo vichache ikilinganishwa na Idadi kubwa ya Wanafunzi walioandikishwa.

 Ndugu Kaseko amewaomba wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kuunga Mkono Sera ya Elimu Bure kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa kujitoa kusaidia jamiI zinazotuzunguka.

 Baada ya Makabidhiano hayo Afisa Elimu Kata hiyo ya Ibondo Ndugu Janerose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo wa Madawati, Madirisha na Katoni mbili za Madaftari.

 Na kwa upande Mwingine Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Emmanuel Mashili amemshukuru Diwani wa Kata hiyo Mh. Mathias Henyenge ambaye pia ni rafiki wa Ndg. Kaseko kwa Juhudi zake kubwa za kuwatumikia wananchi wa Kata ya Ibondo. 

Vichwa vya magazeti ya leo.