Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Ijumaa, 28 Aprili 2017

Ajira:Taarifa za kuitwa kazini kwa madaktari waliokuwa wamekidhi vigezo kwenda kufanyakazi nchini Kenya.

Vyeti Feki: Rais Maguli Afuta Zaidi ya Ajira Elfu 9 Za Walioghushi Vyeti

Rais  Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza Wizara ya Fedha kufuta mara moja ajira za  watumishi wa umma 9,932 waliobainika kughushi vyeti, kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma.

Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu  wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.

Wakuu wa Mikoa, Wilaya Wanusurika Sakata la Vyeti FEKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bora Mhe. Angellah Kairuki amebainisha baadhi ya mambo waliyokuwa wameyapa kiupambele katika zoezi zima la uhakiki wa vyeti feki kwa kusema zoezi halikuweza kuhusika na viongozi wa kisiasa.

Kairuki amebainisha hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa uhakiki wa vyeti feki kwa Watumishi wa Umma lilioendeshwa na Serikali kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.

"Zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa kama Wabunge, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa sababu kwa mamlaka za uteuzi wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika tu...Watumishi 9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi sawa na asilimia 2.4 . Wenye vyeti vya utata ni 1,538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia 94...Hatua hazitachukuliwa kwa wenye vyeti feki tu, bali hata kwa wanaohusika kutengeneza vyeti hivyo". Alisema Kairuki

Aidha Mhe. Kairuki amewataka wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya kughushi waache mara moja kwa kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka saba.

Pamoja na hayo, Kairuki amepongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua kushughulika na zoezi hilo na kulimaliza kwa awamu moja tofauti na nchi nyingine zilichukua awamu tatu huku akitolea mfano wa kwa kuzitaja nchi hizo kwamba ni South Africa na Nigeria.

Kwa upande mwingine,  Rais Dkt. Magufuli amewaagiza Waziri Kairuki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaondoa watumishi wote waliobainika kuwa wanatumia vyeti vya kughushi 'hewa' huku akisisitiza kwamba yeye hawezi kuwasemehe watu walioghushi kwani wataondoka mara moja.

TANAPA watolea ufafanuzi taarifa zilizosambaa mitandaoni kuhusu Mwalimu wa Chuo Sinon Dar kujeruhiwa na Simba.


CUF Lazima Kuchafuke: Wabunge Upande wa Maalim Wamepanga Kufanya Usafi Ofisi Kuu, Kambi ya Lipuma Imejipanga Kuwazuia

Wapinzani wawili katika mgogoro wa uongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Profesa Ibrahim Lipumba sasa wamefikia pabaya baada ya kuamua kupambana kuichukua ofisi ya makao makuu iliyopo Buguruni.

Kwa sasa ofisi hiyo inatumiwa na Profesa Lipumba, ambaye uamuzi wake wa kurejea madarakani mwaka mmoja baada ya kujiuzulu uenyekiti na nyadhifa nyingine zote, unapingwa na kundi lililopanga kuzichukua ofisi hizo Jumapili.

Jana, kundi linalompinga Profesa Lipumba lilitangaza kuwa litakwenda ofisi hizo Jumapili kwa ajili ya kusafisha “kila kitu ambacho hakitakiwi kiwepo”, lakini mwenyekiti huyo amesema ameshajiandaa kukabiliana nao na ameripoti suala hilo polisi.

Profesa Lipumba alisema hayo jana, ikiwa ni siku moja tangu Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limtake ajitokeze kuzungumzia kitendo cha walinzi wa CUF kuwashambulia waandishi wa habari waliokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wa chama hicho Kinondoni.

Profesa Lipumba alikuwa akiwajibu wabunge wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif waliowaambia wanahabari katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana kuwa wamepanga kwenda ofisi za Buguruni Jumapili ijayo na wataungana na wanachama wengine kufanya usafi.

“Tulianza kufanya usafi soko la Buguruni, tukamalizia katika ofisi yetu. Kwa hiyo katika hali nzuri, hatuhitaji wabunge wasumbuke kufanya usafi siku hiyo,” alisema Profesa Lipumba

Profesa Lipumba alisema watu hao hawana nia ya dhati ya kufanya usafi, bali wamepanga kufanya vurugu katika ofisi hizo kwa kushirikiana na watu wa chama kingine cha upinzani.

“Wanataka kuleta vurugu ili CUF ionekane na taswira mbaya kwa Watanzania. Naomba wanachama waepuke mtego huu, namshauri (Mbunge wa Temeke, Abdallah) Mtolea akafanye usafi huo Temeke mbona kuna masoko mengi tu machafu?” alisema.

Awali mjini Dodoma, wabunge wanaomuunga Maalim Seif walisema watakwenda na vifaa vya usafikuondoa kila uchafu watakaoukuta

“Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao hawamkubali Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti, wameamua kwenda kufanya usafi kwenye ofisi zao za Buguruni, ofisi kuu ya CUF Buguruni,” alisema Mtolea akiwa ameambatana na wabunge wenzake katika mkutano na waandishi uliofanyika chumba cha habari cha Bunge.

“Na hatua hii imekuja baada ya kuona ofisi ile inatumika vibaya. Imekuwa ndio kijiwe cha wahuni kupanga matukio ya kihalifu. Kwenda kuvamia mikutano, kwenda kuwavamia watu na kadhalika. Sasa sisi kama wanachama tumeona hatuwezi kuiacha hali hiyo iendelee.”

Aliwataka wanachama kutoka maeneo ya Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine wafike kufanya usafi huo.

Alipoulizwa aina ya uchafu wanaoenda kuuondoa, Mtolea alijibu “ni kitu chochote ambacho hakiko mahali pake” na kwamba hata Profesa Lipumba hayuko mahali pake.

“Tangu Msajili amtambue Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti, hatujawahi kwenda katika ofisi yetu ya Buguruni, matokeo yake ofisi hiyo imekuwa na uchafu mwingi na kuwa pango la wahuni,” alisema Mtolea.

Alipoulizwa uwezekano wa kutokea vurugu, Mtolea alisema hawajiandai kufanya fujo, bali kufanya usafi.

Kuhusu kesi iliyopo mahakamani kuhusu mgogoro huo, alisema ile inapinga msajili kumtambua Lipumba na haizuii kusafisha ofisi yao.

Alisema hawaendi kuteka ofisi hizo, bali wanakwenda kwenye ofisi zao hivyo hawahitaji kuomba ruhusa kwa mtu yeyote.

“Ofisi ni chafu, sisi tunataka tukaisafishe kwa sababu imekuwa sehemu ya kupanga mipango mibaya kwa mustakabali wa chama,” alisema.

Akiweka msisitizo wa jibu hilo, Mbunge wa Chambani, Yusuf Salim Hussein alisema hakuna silaha ya moto inayoshinda nguvu ya umma.

Awali, wabunge hao walitoa tamko la kuunga mkono tamko la TEF kuhusu kulaani kitendo cha wafuasi wa Profesa Lipumba kuwashambulia waandishi wa habari.

Mnadhimu wa chama hicho na Mbunge wa Malindi, Ally Salehe alisema TEF imetoa tamko zito la kutaka waandishi wa habari kufanya kazi kwa usalama na uhuru.

“Na isiwe TEF tu, tunataka watu wote waliokerwa na tukio hilo watoe tamko la kulaani,” alisema.

Kuhusu tamko la TEF, Profesa Lipumba alisema atatoa tamko kuhusu suala hilo ifikapo leo.

“Mimi ni muumini wa demokrasia. Hapa ninavyoongea na wewe nipo katika hatua ya mwisho ya kumalizia kuandika barua kuelekea TEF ambayo itafika kati ya leo (jana) jioni au kesho,” alisema.

Hata hivyo, alisema mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma, Abdul Kambaya alitoa tamko kuhusu tukio hilo.

Katika tamko lake, Kambaya alisema mmoja wa watu walioshiriki kushambulia mkutano ni mlinzi wao na kwamba alikuwa katika doria kudhibiti wanachama wanaofanya mikutano hotelini. 

CCM: Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini.
 
Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa  jana mchana
 
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.
 
Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta.
 
"Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo(jana)  saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake," alisema Mjengi na kuongeza:
 
"Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani," alisema Mjengi.
 
Alipohojiwa zaidi, Mjengi alikataa kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.

MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ,Tumaini Sylivanus akitoa maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa wafanyakazi wa Mgodi huo pindi wapatapo matatizo.
Mmoja wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa moto pindi yatokeapo majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la modi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Kilimanjaro.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Daktari kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara Cyprian akionesha picha na maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi.
Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

 
Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Waziri Masauni: Waliolipua Bomu Nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar ni Viongozi wa CUF

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema viongozi waandamizi wa chama cha wananchi (CUF) ndiyo walihusika na tukio la kulipua bomu katika nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu

Mhe. Masauni alieleza hayo Bungeni Jijini Dodoma jana pindi alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Gandu kupitia tiketi ya (CUF) visiwani Pemba, Mhe. Othuman Omary Hajji alipotaka kujua kwanini mpaka leo hajizachukuliwa hatua stahiki kwa wafuasi wa CCM waliochoma nyumba za wanachama wa CUF huko visiwani Tumbatu, huku akidai serikali iliyopo madarakani siyo halali ni haramu kwa kuwa Jeshi la Polisi lilichangia kumuweka madarakani Dkt. Ali Mohamed Shein.

"Ni kweli baada ya uchaguzi mkuu baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo chake, viongozi walijitokeza kuhamasisha wananchi kufanya mambo yanayokiuka sheria za nchi yetu.

"Kuna matukio mbalimbali yalijitokeza ikiwemo kuchomwa moto nyumba, kuchoma mashamba, kurusha mabomu ikiwemo nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi wa Zanzibar ambayo kwa uchunguzi uliofanyika mpaka sasa, watu waliokamatwa kwa kuhusika urushaji bomu katika nyumba ya Kamishna ni viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF)". Alisema Masauni
Pamoja na hayo, Masauni alisema Jeshi la Polisi limeshakamilisha uchunguzi wake na jalada la mashtaka  lipo kwa DPP muda wowote kuanzia sasa litapandishwa Mahakamani ili sheria ichukuliwe.

Ray Kigosi afunguka Mambo Mazito kuhusu marehemu Kanumba Kuhusishwa na Uchawi na Freemason

Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa baadhi wa Watanzania ni wanafiki na wamekuwa wakikatisha tamaa watu katika mambo yao kutokana na unafiki wao.

Ray Kigosi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema kutokana na unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi yake.

==>Ray Kigosi ameandika;
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!

2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!

3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.

And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.

Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.

5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.

MWANARIADHA SIMBU APOKELEWA BUNGENI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 27 Aprili, 2017 amempokea mwanariadha na mshindi wa tuzo ya dhahabu kwenye Mumbai Marathon Bw. Alphonce Simbu na kumtambulisha kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma. Bw. Simbu aliongozana  na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Kujenga Taifa ameweza pia kukutana na Mhe. Kassim M. Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Serikali.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 27 Aprili, 2017 amempokea mwanariadha na mshindi wa tuzo ya dhahabu kwenye Mumbai Marathon Bw. Alphonce Simbu na kumtambulisha kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma. Bw. Simbu aliongozana  na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Kujenga Taifa ameweza pia kukutana na Mhe. Kassim M. Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Serikali.
 

Alhamisi, 27 Aprili 2017

Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia ya Tanzania kuingizwa nchini humo.....Zitto Kabwe Aitaka Serikali Ichukue Hatua

Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ‘ ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania ‘.

Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. 

Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. 

Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017

Rais Magufuli: Olewak Atakayethubutu Kuuvunja Muungano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

''Muungano ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano  kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.

Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli  na nchi kavu.

Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.

Kwa mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

''Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla  kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na  kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017

Marekani yaanza kujenga mtambo kuzuia makombora ya Korea Kaskazini

Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju

China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

THAAD ni nini?
  • Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
  • Hugonga kombora la kuliharibu
  • Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
  • Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC
Baada ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika ujumbe huu

"Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….

"Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….

"niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku"

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 27