Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumanne, 9 Januari 2018

BUGURUNI: Bomba la Gesi lalipuka na kusababisha moto mkubwa



TPDC imesema bomba la gesi limelipuka eneo la Mnyamani, Buguruni baada ya wafanyakazi wa Dawasco kulitoboa kwa bahati mbaya wakati wakitengeneza bomba la maji #MwananchiUpdates

Ikulu: Rais Magufuli akutana na Edward Lowasa Waziri Mkuu Mstaafu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.

“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema Mhe. Lowassa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Mhe. Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake katika nchi.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.

“Mhe. Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu, kwa ujumla Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, na mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi.

“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7, amezungumzia juu ya elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za hospitali na mengine” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Januari, 2018

Jumatatu, 8 Januari 2018

BIG NEWS: VIBOKO 12 KWA ATAKAE SIMAMA NA MWANAFUNZI, NA FAINI .........

TAHADHARI
BAKORA ZITAKUHUSU


Kama wewe ni kijana wa kiume usisimame na wanafunzi wa like, ukionekana tu utachapwa viboko 12 au faini Tshs. 10,000

Ukiwa katika kata ya Ihungwe wilayani Sengerema usithubutu kusimama na mwanafunzi wa kike, ukikamatwa utachapwa viboko 12 au faini ya 10,000 baada ya viongozi wa kata hio kupitisha rasmi sheria hio  katika kikao chao cha baraza la maendeleo ya kata kilichofanyika hivi karibuni, kufuatia tatizo la kupata mimba wanafunzi wa kike kuzidi kuwa sugu.

Sheria hio  ndogo imepitishwa ikitanguliwa na agizo la Mkuu wa wilaya ya Sengerema Nd. Emanuel Kipole alieagiza Wanaume watakaokutwa na wanafunzi wa kike  wapigwe bakora 12 au faini ya Tsh.10,000, agizo hilo  alilitoa mwezi oktoba mwaka 2017

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

Jumapili, 7 Januari 2018

NEWS: CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAELEKEA KWENYE.........

CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUUMAPEMA MWAKA HUU 2018.


Habari na, Murtadhwa Elbahsan.

Chama cha Skauti Tanzania kimetangaza upatikanaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, hii ni desturi ya upatikanaji wa uongozi wa Skauti Tanzania.

Kwa kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania, ambacho ndicho chombo kincho piga  kura na kupata viongozi WA juu wa chama hicho, Baada ya kukamilisha mhakato wa upatikanaji wa majina 3 ya skauti mkuu yatakayo pelekwa kwa Mlezi wa Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuteua Skauti Mkuu.

"Kwa sasa chama cha skauti Tanzania kinataraji kufanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wao wa juu, ambapo tarehe rasmi za uchaguzi huo ni 22 Februari 2018 katika ukumbi wa Karimjee" alisema Bi. Eline Kitaly ambaye ni Kamishna Mtendaji wa Skauti

Fomu rasmi ya kugombea nafasi ya skauti Mkuu hii hapa chini......


VIGEZO MAALUM VYA KUMPATA SKAUTI MKUU

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
1. Awe na umri usiopungua miaka 45
2. Awe kiongozi aliyewahi kutoa huduma iliyotukuka kwa
Chama cha Skauti Tanzania na Jamii
3. Awe na ueledi wa mambo ya Skauti
4. Awe miongoni mwa Wakufunzi Wasaidizi (ALTs)
5. Awe na uzoefu usiopungua miaka 15 katika uongozi wa
Skauti Watu Wazima (Adult in Scouting)
6. Awe na Uwezo wa kusimamia na kuendeleza Skauti kwa
ujumla


Eidha kwa sasa Bi. Mwantum B. Mahiza ndio Skauti Mkuu na Kamishna Mkuu wa Skauti ni Ndugu Abdulkarim E. H. Shah.

Chama cha Skauti pamoja na kuwa na Makamishna wakuu wa saidizi pia kuna Naibu Kamishna Mkuu ambaye ni ndugu Rashid K. Mchatta, viongozi wote hao wanamaliza muda wao wa uongozi tangu kuchaguliwa kwaomara baada ya kupatikana viongozi wapya baada ya uchaguzi na kfuatiwa kuteuliwa kwa Skauti Mkuu na Mlezi wa Skauti (Rais wa nchi)


Kipenga cha kumtafuta Skauti Mkuu kimepulizwa, nafasi ziko wazi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Januari, 2018 waweza kujaza fomu kielektronik kwa kubonfya hapa >>>>> https://tzcentenary2017.wordpress.com/2018/01/06/fomu-ya-uongozi-chama-cha-skauti-tanzania/ thttps://www.scout.org/tanzania pia waweza kupata fomu ya uongozi kwa barua pepe ya: szone2012@live.com au dsmscout@gmail.com
Waweza pia kupakua fomu hii kwa https://web.facebook.com/SCF360


Ijumaa, 5 Januari 2018

MTOTO WA MZEE KINGUNGE AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA BABA YAKE ZINAZOSAMBAA MITANDAONI..

Mtoto wa mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombae Mwiru,Tonny Ngombale Mwiru amekana taarifa zinazozagaa mitandaoni kuhusu kifo cha baba yake mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Tonny amefanya mahojiano na waandishi wa habari jioni ya leo na kuwaeleza kuwa baba yake yuko hospitali akipata matibabu baada ya kung’atwa na mbwa hivyo kupata majeraha Kwenye miguu ambayo ndiyo anayouguza hospitalini kwa sasa.

Kuhusu mazishi ya mke wa mwanasiasa huyo ambaye alifariki jana katika hospitali ya Muhimbili Tonny Ngombale Mwiru amesema familia itatoa taarifa mapema kesho baada ya baba yao mzee kingunge kuelezwa na kutoa maelekezo kama baba mzazi na kiongozi wa familia hiyo.

Jumatano, 3 Januari 2018

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA 2018



Baraza kuu la Taifa la Chama cha Skauti Tanzania litakuwa na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi utakaofanyika tarehe 22.02.2018 Dar Es Salaam katika ukumbi wa Karimjee Hall.

Wajumbe halali watakaohudhuria Mkutano huu ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama 2017 Ibara 5.2.1 na 5.2.2. Wajumbe wote watatakiwa kuripoti Makao Makuu ya chama tarehe 22.02.2018 saa 01:00 asubuhi. Wajumbe husika toka Mikoani ni sita
(watatokana na Mkutano Mkuu au kwa ushauri kati ya Bodi na Kamati Tendaji ya Mkoa).

Mkutano utakuwa na Ajenda zifuatazo:
a. Kuthibitisha mihtasari ya mikutano ifuatayo:
i. Mkutano Mkuu wa Baraza wa tarehe 25.08.2015
ii. Mkutano Maalum wa Baraza wa tarehe 28.07.2017
b. Yatokanayo na mikutano fuatayo:
i. Mkutano Mkuu wa Baraza wa tarehe 25.08.2015
ii. Mkutano Maalum wa Baraza wa tarehe 28.07.2017
c. Taarifa ya Kamishna Mkuu ya mwaka 2016 hadi 2017
d. Taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016 na 2017
e. Mapendekezo ya Mabadiliko ya P.O.R ya Chama cha Skauti Tanzania.
f. Uchaguzi wa viongozi wa Chama

Sifa na fomu za kugombea nafasi tajwa zinatolewa na kurejeshwa Makao Makuu ya chama kuanzia tarehe 02 Januari, 2018 hadi 15 Januari, 2018 . Pia zinapatikana kupitia www.tanzaniascouts.org / www.scout.org/tanzania / www.DaresSalaamlocalscout.blogspot.com na elbahsan.blogspot.com Mwisho wa kurejesha fomu
Makao Makuu ni tarehe 15 Januari, 2018 saa 10:00 Jioni.

Wajumbe watajigharamia usafiri na malazi . Chama kitarejesha Tshs 100,000/= kwa
kila mjumbe kama posho ya kujikimu.

Wako katika Skauti
Eline Kitaly
KAMISHNA MTENDAJI

soma Hapa kwa habari zaid