LAWRENCE HAMPHREY MHOMWA HATUNAE TENA.
Chama cha Skauti Tanzania kimepatwa na pigo kubwa baada ya kufariki aliyekuwa Kamishna Mkuu na mkufunzi wa chama, ndugu Lawrence Humphrey Mhomwa.
Enzi
ya uhai wake Marehemu Lawrence Hamphrey Mhomwa (wa pili kutoka kushoto)
akiwa na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza kuu wakifuatilia
jambo kwa makini, ulifanyika tarehe 05 Januari 2013 katika ukumbi wa Don Bosco UpangaDar Es Salaam.
Kwa mujibu wa msemaji wa wana-familia ya marehemu Mhomwa alisema, "Mpendwa Lawrence alifariki tarehe 20.03.2015"
Marehemu Lawrence Mhomwa, mpaka anafariki alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC).
Marehemu
ndugu Lawrence Hamphrey Mhomwa alizaliwa katika kijiji cha Ng'ombo
Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tarehe 18 Desemba 1958.
Marehemu
Lawrence aliamia jijini Dar Es Salaam na kuishi na mjomba wake ndugu
Gabriel Matao na kuanza Elimu ya Msingi katika Shule ya Uhuru
Mchanganyiko mwaka 1967 hadi mwaka 1974 alipofaulu na kujiunga na Shule
ya Sekondari ya Azania mwaka 1975 hadi 1978.
Skauti kikosi maalum cha pared wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Lawrence Humphrey Mhomwa kuelekea kanisani kwa ibada.
Kamishna
Mkuu wa Skauti Mhe. Abdulkarim Shah (Mb) alimuelezea marehemu Mhomwa
alikuwa mtu shupavu na alikuwa kiongozi pamoja na mkufunzi wake katika
nishani mbalimbali za Skauti alizopata Mhe. Shah, pia Kamishna Mkuu Mhe.
Shah aliendelea kusema, " marehemu ndungu Lawrence Mhomwa alijiunga na
Chama cha Skauti Tanzania mkoa wa Dar Es Salaam tangu alipokuwa katika
shule ya Msing ya uhuru Mchanganyiko miaka ya 1970 na kuendelea na
shughuli za Skauti hadi alipoingia katika shule ya Sekondari ya Azania
mwaka 1975.
Kamishna
Mkuu Mhe. Shah (Mb) aliendelea kusema, " Akiwa shuleni Azania Marehemu
Lawrence Mhomwa aliongeza juhusi na maarifa zaidi katika shughuli za
Skauti na kutunikiwa nishani ya Kwanza ya Skauti (First Class) tarehe
03.09.1975, ambapo pia alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kikosi (Patrol
Leader), na baadae kuwa kiongozi wa kikundi (Troop Leader).
Mhe.
Shah (Mb) alizidi kufafanua kuhusu marehemu Lawrence Mhomwa kuwa, baada
ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari katika Shule ya Azania na huku
akifanya kazi, Marehemu Lawrence Mhomwa aliendelea na shughuli za Skauti
hadi kuteuliwa kuwa Kamishna wa Skauti Wilaya ya Kinondoni mwaka 1980
hadi 1985.
Marehemu Lawrence Mhomwa alishika nyadhifa mbali mbali.
Mwaka
1986 hadi 1990 alikuwa Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam, mwaka
1991 hadi 2001 aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi Mafunzo,. Makao
Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania.
Mwaka
2002 hadi 2005 aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi Programu za
Vijana, makao makuu ya Chama cha Skauti Tanzania na mwaka 2008 hadi 2012
aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania ambapo baada
ya hapo alimwachia Mhe. Abdulkarim Shah (Mbunge wa Mafia)
Enzi ya uhai wake, Marehemu Lawrence Humphrey Mhomwa akiwa katika utendaji kazi wa Skauti ofisini kwake Chama cha Skauti Tanzania. |
Msemaji
wa familia ya marehemu alizungumzia kuhusu marehemu katka shughuli zake
za kazi, msemaji huyo alisema, Marehemu ndugu Lawrence Humphrey Mhomwa
baada ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari aliajiriwa na Hotel ya
Kunduchi Beach iliyopo jijini Dar Es Salaam na kufanyakazi kama Mhudumu
na baadae kuhamishiwa Idara ya Utunzaji bidhaa (store keeper) mwaka 1978
mwishoni hadi mwanzoni mwaka 1980.
Tarehe
30 Julai 1980 aliajiliwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kama
mhudumu wa ndani ya ndege (cabin crew). Mwaka 1986 kutokana na utendaji
wake mahiri wa kazi, alipandishwa Cheo kutoka Muhudumu Mkuu (Senior crew
hadi kuwa Senior Fight Pursers).
Marehemu
Lawrence Mhomwa alifanyakazi katika Idara mbalimbali ndani ya Shirika
la ndege la Tanzania, ikiwa ni pamoja na Idara ya Mizigo (Cargo
Department) pamoja na Idara Uendeshaji (Operation Department) mwaka
1990.
Aliendelea
kusema kuwa, "Marehemu Lawrence Mhomwa alipata mafunzo mbalimbali
kuhusu masuala ya Usafiri wa ndege na usalama ndani ya ndege. Mafunzo
hayo pamoja na mengine ambayo yalimwezesha marehemu ndugu Lawrence
Mhomwa kupandishwa cheo na kuwa Mkufunzi Mkuu (Chief Instructor) kutoka
chuo cha Wahudumu wa ndege cha Shirika la Ndege la Tanzania.
Skauti mbali mbali waliudhuria maziko ya Marehemu Lawrence Humphrey Mhomwa kama wanavyoonekana katika picha wakiwa katika eneo la makaburi ya Kinondoni. |
Msemaji
kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Shirika la Ndege la Tanzania,
alimuelezea marehemu Lawrence Mhomwa kuwa, "Alikuwa mtu mahili sana, na
kutokana umahili wake na mafunzo thabiti aliyoyapata kutoka katika Chama
cha Skauti Tanzania pamoja na Shirika la Ndege la Tanzania, tarehe 13
Februari 1988 wakati ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya
Boeing 737 ilipotekwa ikiwa safarini kutoka Dar Es Salaam kwenda
Kilimanjaro, marehemu ndugu Lawrence Mhomwa ambaye alikuwa ndani ya
ndege hiyo kwa siku hiyo, alifanya kazi kubwa sana ya kuwatuliza abiria
walikuwa wanataka kupambana na watekeji wa ndege hiyo".
Msemaji
huyo aliendelea zaidi kusema, "Kutokana na ushupavu na ujasiri wake
huo, tarehe 26 Aprili 1989 katika sherehe za Muungano alitunukiwa
NISHANI YA JUU YA USHUPAVU, na Rais wa awamu ya pili Mheshimiwa ndugu
Ali Hassan Mwinyi, katika viwanja vya Ikulu jijini Dar Es Salaam".
Kwa
maelezo mengine ambayo Dar Scout Media iliyapata kutoka kwa msemaji wa
familia ya marehemu Lawrence Mhomwa kuwa, Marehemu Lawrence Mhomwa pia
aliwai kuwa Katibu wa Chama cha Wafanyakazi (COTWU) tawi la Uwanja wa
Ndege wa Dar Es Salaam mwaka 2005 hadi 2011 na baade kuendele kuwa mmoja
wa Wajumbe wa Chama hicho.
Pia,
wahudumu wa ndani ya ndege wa Shirika la Ndege la Tanzania,
walimuelezea marehemu Lawrence kuwa alikuwa mtu wa watu na wa kuigwa
hakika watamkosa wa kuweza kumlinganisha.
Hadi alipofariki tarehe 20 Machi 2015Marehemu
Lawrence Humphrey Mhomwa alikuwa anashikiria wadhifa wa Mkufunzi Mkuu
(Chief Instructor) katika Chuo cha Wahudumu wa Ndege wa Shirika la Ndege
Tanzania.
TAARIFA ZA UGONJWA HADI KUFARIKI KWAKE
Matatizo
ya kuugua kwa marehemu Lawrence Mhomwa yaliaanza kiasi cha wiki nne (4)
zilizopita, akisumbuliwa na matatizo ya maumivu katka koo.
Marehemu
alikuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Regency na TMJ zote za
jijini Dar Es Salaam na alikuwa akiendelea vizuri tu hadi usiku wa
tarehe 19 Machi 2015 hali yake ilipobadilika ghafla, na asubuhi ya
tarehe 20 Machi 2015 marehemu aliomba familia yake impeleke kwa
Mchungaji kwa ajili ya maombi, akiwa njiani kuelekea kwa Mchungaji, hali
yake ilibadilika tena, na familia kuamua kumpeleka hospitali ya
Mwananyamala ambapo alifariki siku hiyo mchana.
Marehemu
atakumbukwa daima kwa umahiri wake na utendaji kazi wake. Taasisi hizi
mbili za Chama cha Skauti Tanzania na Shirika la Ndege la Tanzania,
ambapo muda wote wa maisha yake amekuwa akizitumikia.
Marehemu Lawrence Humphrey Mhomwa ameacha Mjane na watoto wanne (4).
PICHA MBALI MBALI KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU LAWRENCE MHOMWA
MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU LAWRENCE HUMPHREY MHOMWA MAHALA PEMA PEPONI, AMIN.
Chanzo cha habri
- Dar Scout Media
- Scout Chat
- +255-655-095559
- Scout Breaking News
- +255-755-095559
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 688 090 423
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania