Na.Murtadhwa Elbahsan / Vero
Ignatus
Siku ya
mabalozi wa usalama barabarani (RSA) imefanyika Kitaifa mkoani Dodoma ambapo Naibu
waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni amekuwa mgeni rasmi, shughuli hiyo imefanyika katika
viwanja vya mashujaa na imewashirikisha mabalozi mbalimbali Tanzania bara na
Visiwani.
Mwenyekiti
wa mabalozi wa usalama Taifa John Seka amesea kuwa lengo kuu la siku hiyo ni
kuweza kuleta uhamasishaji kwa wananchi ili waweze kupata elimu ya usalama barabarani
na wasione ni jukumu la jeshi la polisi peke yake, kukuza mahusiano na jeshi la
polisi pamoja na mabalozi kufahamiana
zaidi na kuwapongeza mabalozi kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya ya kujitolea.
Kwa upande
wake kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani
ambae pia ni katibu wa Baraza la usalama barabarani Taifa DCP Mohammed Mpinga amesema kuwa takwimuza vifo na majeruhi
zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zinaathirika sana na tatizo hili hivyo bado
tunalo jukumu kubwa la kupingana na
ajali za barabarani
Ameainisha
takwimu za ajali kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017 zimepungua kwa asilimia 44 vifo vimepungua 13% majeruhi 30% ambapo wa
asilimia kubwa RSA inahusika kwa kiwango kikubwa kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi changamoto kutambua juhudi za usalama barabarani
wanaojitole.
Mpinga ambae
pia ni mlezi wa( RSA)amewapongeza
mabalozi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kukabiliana na ajali za barabarani kwa
kuonya kukaripia pale wanapoana mwenendo mbaya wa madereva pamoja na kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani
“ Muendelee
kujitoa kama vile ambavyo mnavyojitoa kwani mnalirahisishia kazi jeshi ,mmekuwa
mkiokoa maisha ya watu wasife kwa uzembe kwaajali za kujitakia “alisema .
Amezitaja
changamoto zinazowakabili ni pamoja na vifaa vya lkutendea kazi,ubovu wa
barabara na miundombinu,ukosefu wa alama za barabarani,utashi wa kisiasa ,wadau
wanaona suala la usalama barabarani siyo la kwao na haliwahusu.
Mkuu wa
kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi
Boniface Ndozero amesema kuwa mambo
mawili lazima yazingatiwe, “ni vyema kuzingatia na kufuata alama za usalama
barabarani yote yakizingatiwa ajali zitapungua kabisa” amesema kuwa jeshi lapolisi
nchini kitengo cha elimu limejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoitoa inawafikia walengwa pamoja na hayo amesema
jeshi la polisi limejipanga kutoa elimu
kwa wanafunzi mashuleni kuhusu elimu ya usalama barabarani
Kwa upande
wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa wanamipango endelevu katika mji wa Dodoma ili ujio wa serikali usije ukaongeza vifo na
ajali kwani wamejipanga kuthibiti ajali za barabarani
Ikumbukwe
kuwa RSA imesajiliwa rasmi mwaka 2014 kama taasisi isiyo ya kiserikali ikiwa na
wanacham 10 hadi sasa wapo zaidi ya 60,000 kwenye majukwaa ya mitandao wa
kijamii (Whatsap, Facebook, Twitter, Instagram nk.), wapo wakurugenzi 8, kanda
5ambazo ni kanda ya kusini, kanda ya kati, kanda ya kaskazini ,kanda ya
mashariki,kanda ya ziwa na kanda ya nyanda za juu kusini, wapo maadimini 20
kwenye majukwaa hayo ya mitandao ya kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni