Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumamosi, 18 Novemba 2017

IJUE RSA NA HISTORIA YAKE

HISTORIA KWA UFUPI
Hapo zamani za kale palitokea kuwapo na kundi moja la wananchi. Kundi hilo lilijiunga pamoja kwenye mtandao wa Whatsapp. Malengo mojawapo ya kundi hilo ni kupashana habari za barabarani kwa minajili ya kupita mustarehe barabarani bila vizuizi vyovyote. Lakini uwepo wa kundi hilo pia ulileta fursa ya watumiaji barabara kulalamikia mambo mbalimbali yanayokera barabarani, ikiwamo mashimo, taa zisizofanya kazi, foleni, maonezi ya askari, nk. Kwa kiasi kikubwa hakukuwa na vitu vingi vya kujielimisha au kuelimishana zaidi ya kupashana habari na kushusha lawama na kutaka mambo yarekebishwe.

Mojawapo ya habari zilizo-trend sana kwenye group hilo ni kupashana habari, wapi wapo askari na wanafanya nini? Na hivyo kusaidia madereva kuwakwepa. Wanachama wa kundi walijuzana tochi zilipo, walijuzana mbinu za kukwepa foleni, mbinu za kunegotiate na askari, na hata kuwasema sana tu. Kwa upande mmoja ilisaidia sana waliomo kwenye kundi husika wasikamatwe kiurahisi.
Kwa ufupi ilikuwa kama laws of the jungle ambapo wanyama huishi kwa kuviziana.

Hata hivyo, baadae alikaribishwa katika kundi hilo kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania. Kuingia tu akashambuliwa kama mpira wa kona lakini akavumilia na taratibu akaanza kushawishi mabadiliko. Ilikuwa kazi kubadilisha mitazamo ya watu na kuwageuza kutoka walalamikaji na wakwepa mkono wa sheria kuwa waelimishaji na sehemu ya suluhisho. Yeye mwenyewe alifika wakati akachoka akakiri kwamba lile ni kundi la watu wanaolalamika tu.

Hatimaye siku ikafika, kundi hilo lililoitwa KULIKONI BARABARANI likageuka kuwa Road Safety Ambassadors na hatimaye group kubadilishwa na kuitwa RSA KULIKONI BARABARANI. Na hii ni baada ya kuungana na kundi la Facebook la Nenda kwa Usalama Barabarani December 28,2014.

KUHUSU RSA TANZANIA
RSA Tanzania ilianzishwa rasmi tarehe 28.12.2014 baada ya kufanyika mkutano mkubwa wa wanagroup la NENDA KWA USALAMA BARABARANI lililokuwepo facebook tangu 17.12.2013 mwanzilishi wake akiwa Augustus Fungo. Katika mkutano huo wa december 28.2014 mojawapo ya waalikwa walikuwa ni wanakundi la whatsapp liitwalo KULIKONI BARABARANI likiongozwa na bwana Jackson Kalikumtima. Makundi yote haya mawili yaani KULIKONI BARABARANI NA NENDA KWA USALAMA BARABARANI yaliazimia kuunngana na kuunda mtandao wa wana usalama barabarani unaoitwa RSA TANZANIA.

Kabla ya kukutana hiyo December 28, kamati ndogo ya watu wanne ikiongozwa na Augustus Fungo, iliundwa na kwenda kuuza wazo la kuwa na mkutano kwa jehsi la polisi kitengo cha usalama barabarani. Kikao cha kwanza cha kuuza wazo kilifanyika kwa Staff Officer wa Polisi Trafiki SACP Johansen Kahatano. Baada ya yeye kukubali wazo hili, alimjulisha Kamanda Mpinga, ambaye naye aliliona ni wazo zuri. Hivyo kwa pamoja tukakubaliana kuwa tarehe 28 tuwe na mkutano. Ni katika mkutano huu ndipo viongozi wa kwanza wa RSA walichaguliwa. Viongozi hao ni 

  1. Mwenyekiti wa RSA Bw. John Seka
  2. Katibu Bi Asina Omary na 
  3. Admin1 bwana Augustus Fungo.
Viongozi hawa walipewa dhamana ya kuhakikisha mtandao wa usalama barabarani unakua na kuwafikia watu wengi, na baadae unasajiliwa kuwa taasisi kamili inayotambuliska kisheria.
Katika mkutano huu, wajumbe walimuomba Kamanda Mpinga kuwa mlezi wa mabalozi wa usalama barabarani na Kamanda Kahatano kuwa Mlezi msaidizi. Majukumu ambayo waliyakubali.
Tangu wakati huo tunawaheshimu makamanda hawa kama walezi wetu, na pia makamanda wa polisi trafiki mikoa tumewafanya kuwa walezi katika ngazi ya mikoa, ila ni pale watakapokuwa wameridhia.


Tangu wakati huo RSA TANZANIA imekuwa na mahusiano mazuri na ya karibu sana na jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani. Na mara kwa mara hufanya vikao na wakuu wa kikosi hicho katika ngazi mbalimbali.


WADHAMINI WA RSA TANZANIA
1. Augustus Fungo (IFM)
2. Jackson Kalikumtima(Private Sector)
3. Ally Nurdin (Unilever Tanzania)
4. Gibson Urassa (UNHCR)
5. Mohammed Mpinga (Police Tanzania)
6. Johansen Kahatano (SUMATRA)
7. Marlin Komba (Wizara Mambo ya Ndani)
8. John Seka (Law School of Tanzania)
9. Adam Phillip (TIB)
10. Asina Omary (Kitivo cha Sheria, UDSM)


BODI YA WAKURUGENZI - WAKURUGENZI WATENDAJI.
Yaani hawa ni wale waliopo kwenye majukumu ya kila siku ya uendeshaji.
1. Augustus Fungo-Taaluma: Sheria
2. Jackson Kalikumtima-Taaluma: Mhasibu
3. Asina Omary-Taaluma: Sheria
4. John Seka-Taaluma: Sheria
5. Ally Nurdin(Six)-Taaluma: Transport and Logistics


KANUNI ZETU ZA MIJADALA HIZI HAPA CHINI (KANUNI KUU 20 ZA RSA TANZANIA)


Katika majadiliano yoyote inayoendeshwa katika majukwaa ya RSA, yawe ya mtandaoni au ya nje ya mtandao, kila RSA atazingatia kanuni na miongozo ifuatayo:

1. HABARI SAHIHI:
Hairuhusiwi kuandika habari yoyote isiyo ya ukweli ama ya kufikirika tu na kuipa uhai kuwa ya kweli.

2. UHAKIKA WA TAARIFA:
 Thibitisha taarifa kabla hujaituma na kama huna uhakika sema “sent as received, for verification”au “Habari hii Haijathibitishwa”. Hapa utaeleweka kuwa unataka jambo lifuatiliwe kujua ukweli wake na kwamba wewe si chanzo halisi cha taarifa.

3. UKAMILIFU WA TAARIFA:
 Ripoti tukio kwa kutoa taarifa inayojitosheleza kwa kutaja nani muhusika (jina/namba ya gari/uelekeo), nini kimetokea, wapi limetokea, na ungependa nini kifanyike.

4. HABARI ZILIZOKATAZWA:
Ni marufuku kupost habari zinazohusu siasa, vichekesho, matangazo ya kibiashara, michezo, muziki, dini au habari binafsi labda kama zimetokea barabarani mf.ajali, homa, kuibiwa, breakdown, na kubambikiwa kosa/jinai. Kama huna hakika na habari tafadhali, mtumie admin inbox kwanza.

5. KUHUSU SALAMU:
 Unapoingia kundini kila siku kwa mara ya kwanza, unaruhusiwa kutao salamu na kisha kuendelea kutoa habari. Mf. Habari za asbh rsa, njia ya makongo iko shwari, au hapa Arusha kuja jama maeneo ya sekela.

6. TAARIFA ZA KIPAUMBELE:
 Taarifa tunazozipa kipaumbele hapa ni zinazohusu msongamano wa magari ili kuwasaidia TCC kujua kwa kuelekeza nguvu kazi; ajali; ukiukaji sheria barabarani; utendaji mbovu wa askari. Aidha UKIMYA wa muda mrefu bila kutoa taarifa au kucnagia mada kwa mwezi mmoja na Zaidi hatutavumilika.

7. UUNGAJI WA WANACHAMA: Huruhusiwi kumwongeza mjumbe yeyote bila ruhusa ya admin na bila kwanza kumwelezea huyo mjumbe mpya nini kinachofanyika hapa rsa. Aidha mtu anayemwombea mtu mwingine uanachama ni sharti ahakikishe anampa mtu huyo kanuni na azikubali, amweleze kuhusu wajibu wake wa kuwa active, na kuzingatia kanuni.

8. WAJIBU WA RSA:
Kuwa RSA ni kuwa mstari wa mbele katika kutii sheria za barabarani; kukiri kosa na kulipa faini au kuomba radhi; kujitolea; kutoa taarifa za barabarani; kujielimisha na kuwaelimisha wengine. RSA hayuko hapa ili kuwa juu ya sheria au kuwa uchochoro wa kuombea feva bila kuwajibika, pia usitake attention ambazo si za lazima.

9. PICHA:
Hairuhusiwi kuweka picha mbaya za ajali zisizowastahi marehemu. Picha yoyote unayoweka humu au video sharti iwe ina maelezo yanayojitosheleza kuelimisha au kuchukua hatua. Pia si ruksa kurudia rudia mara nyingi kutuma picha hizo hizo au zinazotoa ujumbe mmoja iwapo ulizotoa awali zinajitosheleza.

10. KAULI/LUGHA YA MAWASILIANO:
Lugha ya Matusi, vijembe, siasa hairuhusiwi katika foram za RSA, wala ubishi usio wa hoja. Siku zote usinungĂșnike, lalamika kwa kutoa hoja na ikiwezekana pendekeza suluhisho.

11. TRAFIKI JAMII:
RSA sio Polisi wala jasusi yeye ni trafiki jamii na ataendelea kuwa trafiki jamii kazi kubwa ni kutii sheria, kujielimisha na kuelimisha, na kutoa taarifa na kuchochoe mabadiliko. Hatuhitaji shujaa mfu (dead hero), usihatarishe maisha yako au usalama wako kwa kupiga picha au kushughulika na tatizo/suala lililo nje ya uwezo wako. Toa taarifa tu.

12. UONGOZI:
Rsa inaongozwa kwa sheria na kanuni. Ni marufuku kujiamulia mambo bila kupata Baraka za uongozi yaani Mwenyekiti, Katibu, Mlezi au Admins. Na kwa upande wa matawi ya RSA mikoani, kila tawi litazingatia mamlaka yaliyo kwenye himaya yake na kuheshimu mamlaka ya taifa.

13. RUFAA/MALALAMIKO:
 Ikiwa utaona umeonewa iwe kwa kufungiwa au kukanywa basi unaruhusiwa kulalamika kupitia mmoja wa wanachama ili alifikishe barazani watu waweze kujadili. Vivyo hivyo ukifungiwa unaweza kupitai mjumbe mmoja wapo au admins kuomba msamaha na kuandika ujumbe wa kuomba kurejeshwa kundini, na kwa masharti utakayopewa.

14. MAAMUZI YA ADMINS:
 Wakati wowote na wanapoona inafaa admins wanaweza kuchukua hatua yoyote kwa mwanachama atakayekiuka utaratibu. Hatua zinaweza kuwa onyo, karipio, au kusimamishwa kwa muda. Admins hawaruhusiwi kutofautiana hadharani isipokuwa inbox.

15. SIRI/USALITI:
 kila rsa ana wajibu wa kutunza siri za kundi zin
azohusiana na taarifa za uvunjifu wa sheria za barabarani.
 Kumtaja mtoa taarifa au kuvujisha utambulisho wake kwa mkosaji ni kosa na ni usaliti na yeyote atakayefanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

16. VITISHO:
ni marufuku rsa yeyote kujaribu ama kumtisha mwenzake inbox au kwa sms au kwa simu au njia nyingine yeyote ila kwa sababu tu ya jambo alilolisema au taarifa aliyoitoa humu inayoenda kinyume na maslahi ya mtishaji au mtuhumiwa.

17. MARUFUKU:
Ni marufuku kwa RSA yeyoye kutumia Uanachama wake kwaajili ya kulinda maslahi yake binafsi, kutisha, kudhoofisha juhudi za RSA, kupotosha, kutotii sheria, kuomba upendeleo maalumu, kudhalilisha  au kuhujumu juhudi zozote za RSA.Kufanya hivyo ni kosa na hatua za kinidhamu zitachukuliwa mara moja.

18. UTII WA SHERIA:
Kila RSA atawajibika kikanuni na kisheria kutii sheria za barabarani kwa yeye kuwa mfano wa kuigwa na mwingine. Mathalani pale atakapopigwa faini kwa kosa halali alilolitenda, hatakiwa kubisha bali kulipa, na pale atakapokuwa amesingiziwa kosa ambalo hajalitenda au halieleweki basi ataomba ufafanuzi ngazi kwa ngazi au kutoa taarifa kwa uongozi wa RSA ilia pate kushauriwa na kusaidiwa.

19. MAHUSIANO MEMA:
Siku zote RSA wataishi, kuhusiana na kuheshimiana kama familia, watakuwa tayari kusaidiana na kushirikishana mambo mbalimbali ya kimaendeleo, ya kihuzuni na kifuraha. Endapo RSA anasafiri kwenda mkoa wowote au sehemu yoyote nchini, atajitahidi kuwaarifu na kuwatafuta RSA waliopo eneo analokwenda ili kukuza mahusiano mema na kubadilishana mawazo.

20. ADHABU:
Mtu yeyote akakayekiuka kanuni hizi, kulingana na ukubwa wa kosa, anaweza kusimamishwa jukwaani au kwenye mjadala mara moja na kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ambako suala lake litajadiliwa na kutolewa maamuzi. Utaratibu huu utawahusu wanachama wanaotumia mitandao ya telegram na whatsapp na mwingine wowote unaofanana na huo, kwa wale wa facebook wanaweza kuondolewa moja kwa moja baada ya kupewa onyo na kutotii. Mtu yeyote atakayesaliti harakati za RSA atashughulikiwa kinidhamu na adhabu yake inaweza kuwa kufutwa uanachama au kusimamishwa


MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA








This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni