SKAUTI ISIKWAME POPOTE NA ITUMIKE KWENYE ULINZI NA USALAMA WA NCHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI amewaagiza Wakurugenzi wote wa Manispaa nchini pamoja na Maafisa Elimu kuhakikisha kwamba Uskauti haukwami bila ya sababu za msingi.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo mnamo tareehe 20, mwezi February, Jijini Dar es salaam kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi katika maadhimisho ya siku ya Skauti Duniani ikiwa ni kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani SIR ROBERT STEVENSON SMITHY BADEN POWEL aliyezaliwa terehe 22 Februari mwaka 1857.
Pia Rais MAGUFULI amesema kuwa Serikali yake inaangalia uwezekano wa
kuitumia Skauti katika vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama wa Nchi.
Kwa upande wake Rais wa Skauti Tanzania Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema ni wajibu sasa kwa vijana kujiunga zaidi na Skauti ili kupata MAFUNZO YA UADILIFU yatakayowasaidia kuwa na maadili mema zaidi na kuipenda nchi yao na kuwataka wakurugenzi kuhakikisha Skauti haifi katika Manispaa zao.
Vile vile Profesa Joyce Ndalichako amesema endapo Vijana nchini watajuinga kwenye mafunzo ya ukakamavu watafanya vizuri kielimu.
Kwa upande wake Kamishna wa Skauti Nchini Abdulkarim Shaha amesema mikakati ya skauti Nchini ni kuwalea watoto kimaadili.
TUJIKUMBUSHE.
Mwanzilishi wa skauti Sir Robert Smith Stephenson Baden Powell alizaliwa London uingereza, mtaa wa stanhope, alikua ni mtoto wa 12 kwa baba yake ambae alikua mchungaji, mama yake alikua akiitwa Henrieta Grace Smyth.
Baden Powell alijiunga na jeshi la uingereza mwaka 1876, aliandika kitabu cha Aids to Scouting mwaka 1899,alipanda cheo cha Major General mwaka 1900, na mwaka huo huo alitunukiwa karibisho la kishujaa wakati akirudi London, 1907 Badenpowel alifanya kambi la kwanza la majaribio katika kisiwa cha bahari ya Brown (Nahapo ndio ulikua mwanzo wa Uskauti.)

Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa akikaribishwa katika kambi la mfano la Skauti alipokua katika shereheza kumbu kumbu ya mwanzilishi wa skauti Duniani. |
Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa akioneshwa maeneo yaliyomo kwenye kambi la mfano la Skauti alipokua katika shereheza kumbu kumbu ya mwanzilishi wa skauti Duniani. |
Kijana wa skauti akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea katika kambi la mfano wakati wa sherehe ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa skauti Duniani |
vijana wa skauti wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa skauti. |