Katika kutimiza maazimio ya ushirikishwaji wa Vijana
katika vyombo vya maamuzi ndani ya Chama cha Skauti (WOSM 2014 - 2023) na utekelezaji wa mpango wa
kuanzisha na kuendesha majukwaa ya Vijana (EAZSYF 2014 - 2018), Chama cha
Skauti Tanzania - Mkoa wa Dar es Salaam, wamefanikisha semina maalum ya
kuwajengea uwezo vijana skauti kutoka wilaya zote tatu zilizopo Mkoani humo
kuhusiana na umuhimu wa kua na majukwaa ya Vijana, Daiolojia (Dialogue) na elimu
ya Programu za Wajumbe wa Amani (MoP).
Semina hiyo iliyofanyika huko Chamazi katika ukumbi
wa shule ya Sekondari Chamazi kuanzia tarehe 8 hadi 10 mwezi April 2016 ambapo
ilikua na idadi ya washiriki 15.
Kwaupande
wake Ndugu, Peter Rodgers (Kamishna wa Skauti – Wilaya ya Temeke) ambae pia
alikua mgeni Rasmi katika kufunga Warsha hiyo, aliwataka vijana hao kuzingatia
na kuyafanyia kkazi yale yote yaliyo wasilishwa na wawezeshaji wa warsha hiyo
na kuhakikisha wanafikia malengo yaliyokusudiwa na waandaji wa warsha hiyo,
aliyasema hayo wakati akifunga rasmi warsha hiyo.
Vile
vile Mwenyekiti wa kamati ya Jukwaa la Vijana Skauti Afrika Mashariki Ndugu,
Murtadhwa Rashid nae alisisitiza kuhusiana na uazishwaji na kuendesha majukwa
ya vijana katika wilaya hizo zilizopata nafasi ya kipekee na kujengewa uwezo wa
hali ya juu kutokana na mada zilizo wasilishwa hapo, pia kupitia nafasi hiyo
aliwataka washiriki na waandaji wa warsha hiyo kua mfano wa kuigwa katika Nchi
ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla “Naomba tuitumie fursa hii kwa kua
mfano wa kuigwa na jamii zetu, pia tuweze kuwashawishi na mikoa mengine nchini
waweze kuanzisha na kuendesha majukwaa ya vijana kwa kutumia hatua kuu nne za
kua Wajumbe wa Amani”
Eidha
mwenyekiti wa kamati ya jukwaa la vijana skauti Tanzania Ndugu, Chacha N. Mwita
kwa nja ya sauti (kupitia simu ya mkononi), ametoa wito kwa makamishna wa
skauti ngazi za mikoa na wilaya kuwapa fursa vijana kutumia nafasi yao kwa
kuwashirikisha katika vyombo vya maamuzi na kuwawezesha ili waweze kuunda
kamati na kuendesha majukwaa ya vijana skauti katika mikoa na wilaya zao.
Picha zote na Elbahsan...
|
Viongozi wa kamati ya jukwaa la vijna Dar es Salaam. (kushot ni Makamo Mwenyekiti(Frides Bakengesa), Mwenyekiti (Tito Jackson) na Katibu(Salma Kweka)) |
|
Mwakilishi kutoka (W) Kinondoni Ndugu, Faraji akiwasilisha mada |
|
Mwakilishi kutoka (W) Ilala Ndugu, Abdul akiwasilisha mada |
|
Mwakilishi kutoka (W) Temeke Ndugu, Ramadhan akiwasilisha mada |
|
Washiriki wakisikila mada kutoka kwa muwezeshaji |
|
Washiriki wakipata picha ya pamoja baada ya kipindi cha kwanza |
|
Washiriki wakipata picha ya pamoja baada ya kipindi cha kwanza |
|
Washiriki wakijadiliana jamo baada ya somo |
|
Washiriki wakisikiliza hoja ya mwezao alipokua akiwasilisha kwao |
|
Washiriki wakisikiliza kwa makini kile walichokua wakifunza kutoka kwa muwezeshaji |
|
Washiriki wakisikiliza kwa makini kile walichokua wakifunza kutoka kwa muwezeshaji |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Muwezeshaji akiwasilisha mada |
|
Mwenyekiti akiongea na washiriki wakati wa kufunga warsha hiyo |
|
|
Makamo Mwenyekiti akiongea na washiriki wakati wa kufunga warsha hiyo |
|
|
|
Mwenyekiti akiongea na washiriki wakati wa kufunga warsha hiyo |
|
|
|
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Skauti na aliekua Muwezeshaji (MoP) Ndugu Murtadhwa akiongea na washiriki wakati wa kufunga warsha hiyo |
|
|
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Skauti na aliekua Muwezeshaji (MoP) Ndugu Murtadhwa akiongea na washiriki wakati wa kufunga warsha hiyo |
|
|
Kamishna wa Skauti (W) Temeke, na Aliekua Mgeni Rasmi katika kufunga warsha hiyo Ndugu Peter Rodgers akiongea na washiriki wakati akifunga rasmi Warsha hiyo. |
|
Kamishna wa Skauti (W) Temeke, na Aliekua Mgeni Rasmi katika kufunga
warsha hiyo Ndugu Peter Rodgers akiongea na washiriki wakati akifunga
rasmi Warsha hiyo. |
|
Kamishna wa Skauti (W) Temeke, na Aliekua Mgeni Rasmi katika kufunga
warsha hiyo Ndugu Peter Rodgers akiongea na washiriki wakati akifunga
rasmi Warsha hiyo. |
Imetolewa
na
Kamati
ya Jukwaa la Vijana Skauti - Tanzania.
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 688 090 423
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni