Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

Chakula Cha Mchana Pamoja Na Watoto wa Mtaani.

Chama cha skauti Tanznaia kupitia wilaya ya ilala mkoani Dar Es Salaam  wameanziasha program ya kula chakula cha mchna pamoja na watoto wa mitaani kila wiki, kwa lengo la kuwavuta karibu ili kuwasadia kuondokana na maisha wanayo ishi sasa kwa kuwatafutia fursa mbalimbali zitakazo waendeleza kimaisha na hatimae waje kuwa wazazi bora katika familia zao. 


Vijana wa mitaani kutokea maeneo tofauti wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa skauti upanga makao makuu ya skauti. (Kamishna wa skauti (W) Ilala Bw. Crispin Criss Majia wakwanza kulia, akiwa na naibu wake Bw Piter Powel wapili kushot.)


Kamishna wa skauti (w) ilala akifanya mazungumzo na watoto wa mtaani na kuwafanyia usjili.


vijana wa mtaani wakisikiliza mongezi kutoka kwa kamishna wa wilaya ya ilala


Vijana wa skauti mkoa wa Dar es salaam wakibadilisahna mawazo na wageni wao (watoto wa mtaani)


Kamishna msaidizi wa wilaya ya ilala Bw. Peater Powel akiwanasihi vijana wa mitaani pamoja na vijana wa skauti juu ya athari za kujiweka katika makundi yasiyo faa.


Skaui wakiwahudumia chakula vijana wenzao washio mitaani kama tafrija ya kukutana kwao kila wiki.

Skaui wakiwahudumia chakula vijana wenzao washio mitaani kama tafrija ya kukutana kwao kila wiki.

Vijana wakiwa katika wakati eneo la skauti upanga (makao makuu ya skauti Tanzania) wakipata chakula cha mchana na skauti.

Vijana wakiwa katika wakati eneo la skauti upanga (makao makuu ya skauti Tanzania) wakipata chakula cha mchana na skauti

Kamishna wa skauti wilay ya Ilala mkoani Dar es salaam akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na tukio zima la kuwakusanya vijana waishio mitaani na kuwaweka pamoja ili kusudi kuwasaidia waondokane na maisha waliyo nayo hivi sasa na kuwaanda kuwa raia wema na viongozi bora wa familia zao huko mbeleni.

Mmoja kati ya vijana waishio mtaani akiongea na vyombo vya habari juu yatukio hilo lililo wafanya wawe hapo katika eneo la skauti ikiwa ni pamoja na kuitaka serikali itoe msaada kwao na chama cha skauti kiujumla ili wafikie malengo waliyo ya kusudia kwao. Aidha kijana huyo alieleza juu ya changamoto zinazo wakabili ikiwa ni pamoja na mavazi, sitara(Pahali pa kulala), na chakula. Pia ameiomba serikali kuliangalia kwa makini suala lao na kupatiwa msaada ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea katika maisha. 


Baada ya tukio zima kukamilika vijana wa skauti pamoja na vijana wa mitaani kwa pamoja walijumuika katika kuifurahia siku hiyo kwa kushiriki michezo mbali mbali ya kiskauti pamoja na kuimba kwa pamoja na kuleta udugu wa pamoja kama waishio katika familia moja.


Ilala District Local Scout Association
Have Lunch with Ilala Scout together with Street Children


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni