WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani |
Akizungumza
wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa
sheria.
"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema Mwigulu.
Aliwaomba wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwapata wahusika wa tukio hilo.
Katika
hatua nyingine Mwigulu ameitaka wizara husika kuhakikisha inatoa fidia
kwa ndugu wa askari hao na majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu
kuitoa.
"Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa" aliongeza Mwigulu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa. |
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote
waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola.
Alisema
wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba
washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.
Alisema linapotokea tukio kama hilo kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia kupitia mitandao ya kijamii hivyo
akatoa onyo kuwa watakao bainika na wao watakamatwa kwa kutenda kosa.
Askari
waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni
pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC
Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub.
Miili ya Marehemu (Askari) ikitolewa uwanjani kwaajili ya mazishi |
Miili ya Marehemu (Askari) ikitolewa uwanjani kwaajili ya mazishi |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni