SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI DUNIANI
Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ni siku iliyopangwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukomesha vita, kutoa elimu juu ya amani na kuimarisha haki za binadamu ambayo husherehekewa tarehe 21 Septemba ya kila mwaka.Mwaka huu 2014, Skauti (Tanzania) tutaungana na Mataifa mengine ya Dunia katika kusherehekea siku hii muhimu ikiwa imebeba kaulimbiu isemayo, ‘‘Right of Peoples to Peace”
Lets meet to the summit of Mt. Kilimanjaro with the Peace message.Mh. Abdulkarim Shah (Mb) Kamishna mkuu Chama Cha Skauti Tanzania. |
Utaratibu wa Upandaji Mlima:
Umri:
> Skauti watakaoruhusiwa kupanda Mlima Kilimanjaro ni wale walio na umri wa miaka 12 na kuendelea, wavulana, wasichana na viongozi wao.
Afya:
> Kila mshiriki atahitajika kupima afya yake katika kituo chochote cha afya kujihakikishia kuwa na afya bora kabla ya kupanda mlima.Vifaa vya Kubeba
> Vifaa vya usafi:- Sabuni ya kuogea, sabuni ya kufulia, mswaki, dawa ya mswaki, mafuta ya mgando n.k.
> Mavazi:- Nguo nzito za baridi Masweta, jackets, nguo za michezo, soksi za mikono na miguu, kofia za baridi n.k.
Ada ya Ushiriki:
> Kila mshiriki atawajibika kuchangia kiasi cha Tshs. 150,000/= ambayo itajumuisha gharama za kuingia mlimani, gharama za kupanda mlima, chakula na malazi kwa kipindi chote cha siku za kupanda mlima.
> Gharama nyingine za usafiri kutoka na kurudi katika mikoa husika na ada za kutoka nje ya mikoa zitagharamiwa na mshiriki mwenyewe binafsi.
> Malipo ya kila mshiriki yanahitajika kulipwa kupitia Akaunti ya Chama cha Skauti Tanzania, iliyoko katika Benki ya National Bank of Commerce (NBC) tawi la Samora,
Account Number 012103010625. Baada ya malipo, Makamishna wa Mikoa watawajibika kutuma majina ya Skauti watakaolipa na namba za stakabadhi za malipo ya Bank Makao Makuu ya Chama kwa uthibitisho.
Kuthibitisha Ushiriki:
> Washiriki watahitajika kuthibitisha ushiriki wa kupanda Mlima kwa Kujaza fomu na kuirejesha Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania kwa njia ya barua pepe (Email) kabla ya tarehe 18 Julai 2014 au kupitia kwa Makamishna wa Mikoa.RATIBA:
S/No. TAREHE TUKIO MUHUSIKA
1. 16 - 17 Septemba 2014 Kuwasili Mkoani Kilimanjaro Uongozi wa Skauti Mkoa wa
Kilimanjaro na Uongozi wa Skauti\ Makao Makuu.
2. 18 - 21 Septemba 2014 Kuwasili Kileleni mwa Mlima Skauti wapanda Mlima
Kilimanjaro
3. 22 Septemba 2014 Kurejea chini ya mlima Skauti wapanda Mlima
4. 23 Septemba 2014 Kuondoka Kilimanjaro Skauti wote
Ni mategemeo yetu kuwa Skauti tutajitokeza kwa wingi kuonyesha mshikamano wetu katika kupeleka ujumbe wa Amani kwa njia kupanda mlima wetu Kilimanjaro, Mlima mrefu Barani Afrika wenye kuleta Amani, Upendo na Matumaini pale ambapo hakuna matumaini
Kwa maelezo zaidi kuhusu upandaji mlima, na watakao hitaji fomu za ushiriki {kwenda kusherekea siku ya Amani duniani} tafadhali tutumie ombi hilo la kupata fomu hiyo kupitia :
Mobile: +255 713 295 715
Tell: +255 2222 153342
Fax: +255 2222 1248 807
Email: Tanzani Scout Association
MLIMA KILIMANJARO |
Alhajj. Omar Khatib Mavura Mratibu Messengers of Peace Taifa. |
Murtadhwa Rashid Abdallah Mratibu Messengers of Peace Mkoa (Dar-es-salaam) |
https://www.facebook.com/pages/Messengers-of-Peace-Tanzania-MOPTZ/1408726232704353?ref_type=bookmark
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni