Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 3 Julai 2014

HATIMAE JUKWAA LA VIJANA LAPATA WAJUMBE WA KAMTI KUU TANZANIA. {TANZANIA YOUTH COMMITTEE} 2014-2016

JUKWAA LA VIJANA TANZANIA, {TANZANIA YOUTH FORUM} 28-30 JUNE,2013 BAHATI CAMP-MOROGORO.


          Chama cha Skauti Tanzania chapata uongozi mpya wa jukwaa la vijana "Youth Forum" yenye wajumbe sita (6) chini ya mwenyekiti Bw. Chacha N. Mwita ambae amekabithiwa rasmi jukumu hilo mapema wiki hii baada ya kuchaguliwa na na vijana walioshiriki jukwaa hilo kutoka mikoa tofauti iliyopo nchini Tanzania, uchaguzi huo uliofanyika 28-30 june, 2014 sambamba na kuendeshwa kwa kongamano hilo juu ya maendeleo ya uskauti na vijana wa skauti kiujumla.


Timu iliyoshiriki jukwaa la vijana 


        















         

         Aidha nae Bw. Chacha (baada ya kuchaguliwa kwa nafasi hiyo) aliitaka kamati yake kuwa makini na kuwa tayari kukitumikia chama cha Skauti Tanzania (kwa kutumia nyadhifa walizo nazo kama viongozi wa vijana nchini) kwa hali na mali ili kuhakikisha wanafikia malengo na dhamira ya chama cha Skauti kidunia.
         Pia Bw. Chacha (Mwenyekiti) alitoa wito kwa vijana wa skauti nchini (Tanzania) kuonesha na kuwapa ushirikiano wanakamti hiyo ya jukwaa la vijana la Tanzania iliyoundwa 30 june, 2014  ili kufanikisha utendaji wa kamati hiyo.

       
         Vile vile Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani) alisisitiza juu ya ushirikiano wa vijana (skauti) na kamati hiyo ili kuleta manufaa kwa wana chama (skauti) katika nche yetu na ulimwengu kiujumla. 
          Ndugu katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani Bw. Murtadhwa R. Abdallah aliwaeleza kwa upana zaidi wajumbe walio hudhuria kongamano hilo juu ya masuala ya ujumbe na wajumbe wa amani (Semina fupi elekezi) na kuwataka wajumbe hao waliohudhuria kongamano hilo kuwa wajumbe (mabalozi) wa kulifikisha na kulifanyia kazi suala la ujumbe na wajumbe wa amani katika mikoa yao na kuanza kulifanyia kazi kwa vitendo suala hilo.
Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani)
Sambamba na viongozi hao wa jukwaa la vijana, pia Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini) aliipa baraka kamati hiyo ya jukwaa la vijana nchini na kuwapa wosia wa kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufuata misingi na kanuni za skauti. 
Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini)

        Pia alimalizia kwa kusema kuwa "Jukwaa la vijana ni moja ya chombo kinacho tumiwa katika kufanikisha shughuli za chama, hivyo ni vyema vijana kukitumia chombo hicho katika kuleta mafanikio ndani ya chama..



Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro.

Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini)akitoa somo kwa vijana waliohudhuria jukwaa hilo.



UONGOZI WA KAMATI YA JUKWAA LA VIJANA TANZANIA 2014-2016




Ndugu, CHACHA MWITA 
(Korogwe)
MWENYEKITI

Bi, ANNA EMMANUEL 
(Dodoma)
NAIBU MWENYEKITI
Ndugu, MURTADHWA RASHID
 (Dar Es Salaam)
KATIBU








Ndugu,TITO JACKSON
(DarEs Salaam)
MJUMBE
Ndugu, ALLEN MPANDE
 (Morogor)
MJUMBE
Ndugu, ELAM MOSSES
 (Mbeya )

MTUNZA HAZINA





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni