Zoezi la uchangiaji damu limezidi kuhamasika, leo hii Skauti 27 wa Sekondari ya Baden Powell Memorial na Viongozi wao akiwemo Masha Missungi walimtembelea Skauta Stewart Kiluswa (LT ) katika hospitali ya Muhimbili (Alipo lazwa kwa ajili ya matibabu ) na kuchangia unit 25 za damu.
Damu hiyo ni kwa ajili ya Skauta Stewart Kiluswa (LT ) na wagonjwa wengine. Imehamasisha sana kwa ujasiri wao na jinsi walivyo pendeza kwa sare yao nadhifu ya Skauti.
Wagonjwa, walinzi na wauguzi wamevutiwa sana na kwa kweli wameendelea kukijengea heshima kubwa chama cha skauti Tanzania pamoja na Skauta Stewart Kiluswa (LT ).
Basi tuendelee na moyo wa aina hii popote tulipo.