Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi.
“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya.
“Mtoto
akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa
wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”
Aliongeza,
“Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima
wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na
kweli nimetulia,”
Muimbaji
huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa
Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa
wa moyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni