Kwenye
video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika
TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa
milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘
"Downloads
zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani
kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua
na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini
likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho
hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii
kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"
Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika;
"Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa
niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni