Manara
amesema hayo siku moja baada ya mfanyabiashara , Mohammed Dewji kutoa
kauli ya kusikitishwa na uongozi wa klabu ya Simba kusaini mkataba wa
udhamini wa muda mrefu na Sportpesa bila ya kumshirikisha yeye, ambaye
aliweka nguvu zake nyingi katika klabu hiyo.
“Uongozi
wowote ni Jalala ila uongozi wa mpira ni Dampo, ‘sometimes’ napokea
lawama zisizonihusu, ‘but’ nina moyo wa chuma na nina uzoefu wa kuwa
kiongozi katika tasnia tofauti, kazi yangu ni kuhabarisha umma, mengine
ni kunionea”ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Aidha,
Manara amesema kuwa hakuhusika kwa chochote katika mchakato huo lakini
kwakuwa yeye nikiongozi amesema yuko tayari kupokea lawama zote
zinazoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni