Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha
Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana
mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu.
Nape
Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama
kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali
kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa
serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa.
"Kimsingi
kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake
sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali
ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila
kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo
yakarekebishika" alisema Nape Nnauye
Mbali
na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri
serikali sasa kupitia bunge anasema hawafahamu pia alipokuwa kwenye
Baraza la Mawaziri, alikuwa akifanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni