Shirika
la Umeme, Tanesco limesema hakuna gharama zozote zinazotozwa kwa mteja
anayetaka kubadilishiwa tarifu kutoka juu kwenda chini...
Akizungumza
na wanahabari mwishoni mwa wiki iliyopita, Kaimu Meneja Masoko wa
Shirika hilo nchini, Mussa Chowo alisema mteja anayetaka kubadilishiwa
tarifu hatakiwi kutozwa gharama zozote.
Alisema
wateja wa kawaida kabisa wanatakiwa kutumia tarifu namba nne ambayo ni
lazima matumizi yake ya umeme yasizidi uniti 75 kwa mwezi na gharama za
kila uniti ni sh. 100.
Kundi
ya la pili ni wateja wa tarifu ya pili ambao hutumia umeme wa uniti
sifuri hadi 1,750 ambao hulipia sh. 292 kwa uniti bila kodi ya ongezeko
la thamani (VAT).
“Tunawaomba wananchi kote nchini kuhakikisha hawachajiwi (hawatozwi) malipo yoyote ikiwa wanataka kubadilishiwa tarifu," alisema Chowo.
"Yeyote atakayetendewa hivyo basi ajue ni kosa la jinai na atoe taarifa kwa ajili ya hatua stahiki kwa aliyetenda kosa hilo.”
Alisema
Tanesco imeshatoa elimu kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini hasa ile
iliyopata miradi ya Rea, lengo likiwa ni kuwapa wananchi elimu ya
kutosha juu ya haki zao na matumizi sahihi ya umeme ili kuepuka gharama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni