MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam mapema leo ametembelea
Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya
ofisi hizo kukumbwa na janga la moto uliotokea hapo jana majira ya saa
nne asubuhi.
Viongozi
wengine wa serikali waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa
Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.
Hata
hivyo, tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea
hewani baada ya kupotea siku nzima jana kutokana na hitilafu
iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni