RAIS PROF. JAKAYA KIKWETE KUUTUBIA SKAUTI
MKUTANO MKUU WA BARAZA KUU TANZANIA
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MGENI RASIMI
Wakati Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania ukianza kwa semina elekezi kwa Viongozi wote wa Skauti Tanzania.
Viongozi
wa Skauti kutoka pande zote za Mikoa ya Tanzania Bara na Tanzania
Visiwani waliwasili kuanzia tarehe 12-08-2015 tayari kwa Mkutano Mkuu wa
Baraza kuu la Taifa ambapo utakaofanyika siku ya jumamosi, tarehe
15-08-2015 katika Ukumbi wa Karimjee Dar Es Salaam, ambapo Mlezi wa
Chama cha Skauti Tanzania Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Professor Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasimi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ni Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Prof. Jakaya Kikwete |
Pamoja
na Rais Jakaya Kikwete kuwepo pia watakuwepo viongozi wa Chama cha
Skauti Tanzania, rais wa Chama cha Skauti Tanzania Dkt. Shukuru Kawamba
(waziri wa Elimu na Ufundi), Skauti Mkuu Mheshimiwa Mwantum Mahiza (Mkuu
wa Mkoa wa Lindi), Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim Shah (Mbuge wa
Mafia - anayemalizia muda wake), Naibu Kamishna Mkuu Ndugu Rashid
Mchatta, Mwenyekiti wa Kamati Tendaji Balozi Nicholaus Kuhanga, pamoja
na Ma-kamishna wote wa Mikoa na Wilaya wa Skauti Tanzania.
Katika
mkutano huo ambapo Rais J. Kikwete atachukua nafasi ya kuwaaga Skauti
Tanzania, wito umetolewa kwa wadau na marafiki wa Skauti kujumuika kwa
pamoja katika tukio hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 asubuhi ya tarehe
15-08-2015, Jumamosi katika Ukumbi wa Karimjee Dar Es Salaam.
Chanzo cha habri
- Chama Cha Skauti Tanzania
- Dar Scout Media
- Scout Chat
- +255-655-095559
- Scout Breaking News
- +255-755-095559
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni