Rais Kikwete (Mlezi wa Chama cha Skauti Nchini) afungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Skauti Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania umefanyika
jijini D’salaam kuanzia tarehe 13 Agosti hadi 15 Agosti 2015 katika ukumbi wa
Karimjee.
Mkutano wa Baraza Kuu hufanyika kila baada ya miaka 2 na mara ya mwisho ulifanyika
mwaka 2013 jijini D’salaam, hadi kufanyika tena mwaka huu 2015 D'salaam.
Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu ulitanguliwa na Semina Elekezi kwa wajumbe wote wa
Baraza Kuu, ambao uliaanza tarehe 13 na 14 Agosti 2015 na kufuatiwa na Mkutano Mkuu wa Baraza
Kuu Taifa uliofanyika tarehe 15 Agosti 2015. Wajumbe wa Baraza walianza
kuripoti jijini D’salaam tarehe 12 Agosti 2015 jioni.
Wajumbe wa Baraza Kuu ni pamoja na Makamishna wote wa Skauti wa Mikoa na
Wilaya za Tanzania, Wakufunzi, Viongozi wa Juu wa Chama, pamoja na wageni
wengine waalikwa.
Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu ulifunguliwa na Mlezi wa Chama cha Skauti
Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wengine wa juu wa Chama ni pamoja na Wadhamini
ambao ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu
Mstaafu Salim Ahmed Salim na Baba Askofu Timanywa.
Rais wa Baraza la Chama cha Skauti Tanzania ni Waziri wa Elimu Mheshimiwa Dk.
Shukuru Kawambwa na Makamu wake ni Kaimu Mufti wa Tanzania Alhaji Zuberi,
Muadhama Kadinali Polycap Pengo na Profesa Philemoni Sarungi.
Viongozi wengine wa Juu wa Chama ni
pamoja na Skauti Mkuu wa Tanzania
Mheshimiwa Mwantumu Mahiza, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
Kamishna
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mheshimiwa Abdulkarim Shah ambaye pia
ni Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Taifa
Mheshimiwa Balozi
Mstaafu Nicholas Kuhanga.
Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu pamoja na mambo mengine ulijadili na kupitisha Katiba
ya Chama cha Skauti Tanzania, pamoja na kuchagua wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Taifa.
Picha zote na Murtadhwa El Bahsan
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, akiingia kwenye ukumbi wa Karimjee, wakati alipokwenda kuufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam |
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, akiingia kwenye ukumbi wa Karimjee, wakati alipokwenda kuufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam. |
Kamishna Mkuu, Mbunge, Abdulkarim
Shah, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa Baraza Kuu
la chama hicho, Dar es Salaam.
|
Vijana wa Skauti, pamoja na Skauta wakisikiliza hotuba mbalimbali
zilizokuwa zikitolewa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama
hicho, Dar es Salaam.
|
Vijana wa Skauti,pamoja na kamati ya Utendaji (Makao Makuu)
wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam.
|
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akiteta jambo na Kamishna Mkuu, Abdulkarim
Shah wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama
hicho, Dar es Salaam.
|
Nae Dk. Shukuru Kawambwa, Raisi wa Chama cha Skauti Nchini akizungumza na wajumbe wa Mkutano huo wakati wa ufunguzi aliwaambia kuwa chama kina malengo makubwa mawili, kwanza kuwaendeleza watoto na vijana kupitia mfumo wa Elimu usio rasmi ili waweze kuwa na makuzi bora kiakili, kimwili na kimaadili. Pili kuwaandaa watoto na vijana kuwa wazelendo na nchi yao, hivyo dhimaa hili kubwa na muhimu kwa mustakbali wa Taifa letu.
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akizungumza wakati alipokuwa akiufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama
hicho, Dar es Salaam.
|
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete,
akizungumza wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es
Salaam.
|
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete,
akizungumza wakati alipokuwa akiufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama
hicho, Dar es Salaam.
|
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akizungumza wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es
Salaam.
|
Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akizungumza wakati alipokuwa akiufungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama
hicho, Dar es Salaam.
|
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam.
|
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam jana.
|
Nae Waziri Mkuu mstaafu na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania aliwasihi vijana wote nchini haswa wanachama wa Skauti kuyazingatia yale aliyo yasema Rais Kikwete, pia aliiambia jamii ya watanzania watambue kua skauti inawahusu Vijana wote wa Tanzania na haina ubaguzi wala haihusiani na masuala ya siasa.
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 688 090 423
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni