Na Murtadhwa Elbahsan
Inaelezwa kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye
ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini Tanzania yamefukuliwa
na watu wasiojulikana.
Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano
dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu
za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba.
Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama
watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza
na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa
Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino
yanatishia amani yao
Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu
katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu
wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao.
“Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao
wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina
wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya
na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner.
Aidha alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa
kaburi la Nelson Msogole (50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya
kufariki tarehe 28/3/2011 na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe
20/3/2017na watu wasiojulikana.
“Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji
kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na
kumepiga hatua?”,alihoji Torner.
Alisema Tangu kuanze kuibuka mauaji ya watu wenye
ualbino mwaka 2007 makaburi 22 nchini yamekwisha fukuliwa katika mikoa
ya Mbeya ,Tabora,Mwanza,Mara ,Kagera,Rukwa, na Shinyanga.
Aliiomba serikali ya awamu ya tano iweke mikakati ya
uelewa kwenye jamii kwani huenda hawana uelewa na watuhumiwa wakibainika
waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
“Hiki ni kipimo cha serikali ya awamu ya tano kwa
sauti ya wanyonge kwani kuna baadhi ya watu wanaishi kwenye nchi yao kwa
hofu na unyonge na kuondolewa utu wao hivyo tuna imani serikali itaweka
nguvu kubwa kuliko kipindi cha nyuma”,aliongeza Torner.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza
Alfredy Kapole alisema mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya vifo vya
albino zaidi ya 17 vimetokea tangu mwaka 2007 hivyo aliiomba serikali
kuweka ulinzi mkubwa kwa watu hao kwani wanakiuka katiba ya nchi kwani
kila mtu anastahili kuishi.
Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mara Joseph
Sinda alisema kitendo cha kufukua kinawafanya waishi kwa hofu kubwa na
kuitaka serikali ijaribu kuchunguza chanzo chake ni nini na kuthibiti
kama kwenye madawa ya kulevya na pombe aina ya viroba walivyofanya ili
waweze kuishi kwa amani.
Mwanaharakati kutoka mkoani wa Shinyanga Eunice
Zabroni aliiomba serikali wawaimarishie ulinzi na elimu itolewe kwani
wanaishi kwa hofu kwa kukosekana ulinzi imara kuanzia ngazi ya
vitongoji,vijiji kata na wilaya hadi mkoa.
Picha na Kareny Masasy
Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimelaani
vikali vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino
vinavyoendelea kujitokeza nchini hali inayowafanya waishi kwa hofu kubwa
katika nchi yao.
Katikati ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha
watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza
wakati wa kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho ambapo
walilaani vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia
ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS
mkoa wa MwanzaAlfred Kapole
Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye
ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner ambapo alisema chama hicho
kinaiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli
kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ualbino
Baadhi ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa katika kikao hicho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni