Na. Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan Dar es salaam.
Madereva
wa mabasi makubwa yaendayo mikoani wameaswa kutokuchezea mfumo wa
kufuatilia mwenendo wa mabasi haswa mwendo kasi ,yeyote atakae bainika
ameuharibu hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed
Mpinga katika hafla ya kufunga kampeni ya abiria paza sauti
iliyofanyika katika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi
jirani cha Ubungo ambapo amesema kuwa mwendo kasi ni chanzo kikubwa cha
ajali barabarani
Kamanda
amefafanua kuwa kampeni hiyo imeleta matokeo chanya ambayo imeonyesha
kupungua kwa ajali ukilinganisha na miaka 25 iliyipita nakusema kuwa
Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuthibiti ajali za barabarani .
Amezitaja
takwimu hizo kuanzia mwaka 2015 Desemba ajali zilikuwa 767 , Disemba
2016 ajali zilikuwa 705, ambapo januari 2016 ajali zilikuwa 681 hadi
januari 2017 ajali zilikuwa 525, Februari 2016 ajali zilikuwa 846 ambapo
februari 2017 ajali zilikuwa 455 ,kuna upungufu wa asilimia 46 'ambapo
ajali zinazidi kupungua mwaka hadi mwaka.
Ameendelea
kusema kuwa kwa takwimu hizo hadi sasa Tanzania imepiga kubwa katika
kudhibiti ajali za barabarani na hii ni takribani nusu karne tangia
mwaka 1989.
Vile
vile Kamanda mpinga alitoa vyeti vya pongezi kwa madereva walio
pendekezwa kama madereva bora kwa mwaka 2016 - 2017 ambao ni;
1. AWADH BAWAZIR(RATCO).
2.ALLY ISSA (STAR BUS)
3. MUSTAPHA GHARIB(KIMBINYIKO)
4. DAUDI LWENA(KHANDAHAR).
1. AWADH BAWAZIR(RATCO).
2.ALLY ISSA (STAR BUS)
3. MUSTAPHA GHARIB(KIMBINYIKO)
4. DAUDI LWENA(KHANDAHAR).
5. MENGI KASIKE(SUTCO).
6. MAJURA KAFUMU
6. MAJURA KAFUMU
Kwa
upande wake mratibu na mwenyekiti wa abiria paza sauti Asp.Mosi Ndozero
amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madereva pamoja na wahudumu wa
magari sambamba na kuwaelimisha abiria kufahamu haki zao pia kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona viashiria vya uvunjifu wa
sheria za barabarani ambavyo vinaweza kusababisha ajali na kupoteza
maisha au ulemavu wa kudumu.
Mosi
amesema kuwa mtu anapopata ajali haathiriki yeye peke yake inajumuisha
familia yake pamoja na serikali kuingia gharama kubwa ya kumuuguza huyu
mtu aliyepata ajali,amewataka mabalozi kuendelea kupaza sauti kwa
madereva bodaboda ambao wanapakiza mizigo kuzidi uwezo wa pikipiki
pamoja na wale anaopakia Mishikaki.
Picha na Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni