Makamu
wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu jana amefungua
Tawi la kwanza la Simba mjini Bukoba na kuweza kuwaunganisha Wana Simba
wa hapa Kagera.
Pia katika Uzinduzi huo
wa Tawi ambalo lipo Kashabo pia walikuwepo Wachezaji wa Simba
wakiongozwa na nahodha Jonas Gerald Mkude, Kichuya na Wengine. Piacha na
Faustine Ruta, Bukoba
Pia
wameweza kumshukuru ndugu Omary Makoye, Mratibu wa Tawi wa Klabu ya
Simba kwa kuwatembelea wakiwa katika Mchakato wa kuunda Tawi hilo.
Na
pia wameshukuru kwa msaada aliowapa na ulikuwa ukihitajika kwa muda
huo. Shukrani pia kwa Ndugu Sued Mkwambi kwa kukubali kuwa mlezi wao wa
Tawi.
Makamu
wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburuakiteta na
Wanatawi na wanakagera waliokuwa eneo la Tawi hilo la Kichwabuta.
Mh. Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey
Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na Viongozi wa Tawi la
Kichwabuta lililozinduliwa leo hii mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina
la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu
ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama
mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba.
|
Tawi
hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu
zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na
utaratibu wa Klabu.
Tawi linaongozwa na
Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu,
Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na
Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.
Wadau na Wapenzi wa Simba wakiwa tayari kwa Uzinduzi wa Tawi hilo.
Wakifuatilia kwa karibu Uzinduzi wa Tawi
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu akisaini kwenye Kitabu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni