Mjumbe
wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Kaseko ametembelea
Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema na kutoa Msaada wa Chakula kwa
Wagonjwa wenye hali ngumu ya Maisha & Wanaohitaji msaada kutoka kwa
wasamalia wema.
Akikabidhi msaada huo kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo
Sr. Mariojose kwa niaba ya Wagonjwa wamama na watoto Ndugu Kaseko ametoa
Chakula Mahindi Kilo 100, Maharage Kilo 50, Soya Kilo 50, Sukari Kilo
25, Mafuta ya Kupikia Ndoo moja ya lita 20, Sabuni & Juice Vyenye
thamani ya Tsh. 700,000/
Mjumbe huyo wa Baraza Kuu UVCCM
Mkoa wa Arusha amesema yeye ni mzawa wa Sengerema na amekuwa akitibiwa
katika Hospitali hiyo wakati wote wa utoto wake hivyo anazifahamu sawia
changamoto zinazoikabili huduma ya afya hospitalini hapo na kwamba
ameguswa sana Matatizo hayo hivyo na kuamua kuunga Mkono Juhudi za
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili Watanzania katika sekta ya Afya.
Ndugu Kaseko ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau
mbalimbaliwa maendeleo kuisaidia Serikali kuwaletea maendeleo wananchi
kwani Serikali ina mambo mengi hivyo peke yake haiwezi ni lazima watu
wenye moyo wa kujitolea na wanaopenda maendeleo wajitoe kuisaidia
Serikali inaayoongozwa na Rais Magufuli ambayo ukweli inajikita haswaa
kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo teule ya Wilayaya Sengerema
Sr.Mariojose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo na kusema ni
wachache sana wenye moyo huo na kumuomba aendelee na moyo huo huo wa
kujitolea wa kuwasaidia wenye Shida hasa Masikini.
Katika hatua nyingine Ndugu Kaseko amekabidhi Madawati
Kumi na Tano manne ( 4 ) Katika Shule ya Msingi Ibondo Wilayani
Sengerema. Ndugu Kaseko ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa
Arusha amesema anaunga mkono Juhudi za Serikali ya Hawamu ya Tano Chini
ya Rais Magufuli na Kwamba Elimu bure imekuja na changamoto kedekede
kote nchini na kwamba serikali inastahili kusaidiwa ili kuhakikisha
Elimu bora inatolewa. Ndugu Kaseko ametaja baadhi ya Changamoto hizo ni
Uchache wa Madarasa ya kusomea, Maabara, Madawati, Vyoo vichache
ikilinganishwa na Idadi kubwa ya Wanafunzi walioandikishwa.
Ndugu Kaseko amewaomba wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea
kuunga Mkono Sera ya Elimu Bure kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa
kujitoa kusaidia jamiI zinazotuzunguka.
Baada ya Makabidhiano hayo Afisa Elimu Kata hiyo ya Ibondo
Ndugu Janerose amemshukuru sana Ndugu Kaseko kwa msaada huo wa
Madawati, Madirisha na Katoni mbili za Madaftari.
Na kwa upande Mwingine Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.
Emmanuel Mashili amemshukuru Diwani wa Kata hiyo Mh. Mathias Henyenge
ambaye pia ni rafiki wa Ndg. Kaseko kwa Juhudi zake kubwa za kuwatumikia
wananchi wa Kata ya Ibondo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni