Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Uwekezaji la
Korea nchini Tanzania (KICoT Corporation) leo, Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wajumbe wa
Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania (KICoT Corporation) leo,
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akiimba wimbo wa Taifa pamoja na Mshauri Mkuu wa
Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania (KICoT Corporation), Mhe.
Balozi Mstaafu wa Korea Kusini hapa nchini Kim, Young-Hoon ambaye
alimwambia Mhe. Makamu wa Rais kuwa bado anaukumbuka wimbo wa Taifa la
Tanzania.
Watanzania waliosoma Nchi Korea Kusini wameunga mkono
jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa
kuleta wawekezaji ambao wanataka kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya
nguo, vifaa tiba, uzalishaji wa nishati ya umeme wa jua, kilimo na
katika sekta ya Sanaa,utamaduni na michezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Uwekezaji kutoka Korea Kusini hapa
nchini Kakono David ametoa kauli hiyo wakati anaongoza Ujumbe wa Baraza
la Uwekezaji la Korea Kusini ambao wamekutana na kufanya mazungumzo na
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa viwanda hivyo utatoa
fursa kubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira nyingi kwa
Watanzania na amesisitiza kuwa kwa kuanzia wawekezaji hao wataanza
kuwekeza katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mazungumzo na ujumbe huo wa
Baraza la Uwekezaji Kutoka Korea Kusini amesema amefurahishwa na ujio wa
wawekezaji hao na amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya Tano
inaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji ili kazi ya ujenzi wa
viwanda nchini iweze kwenda kwa kasi inayotakiwa.
Makamu wa Rais amesema ujenzi wa viwanda unaoendelea
kufanywa na wawekezaji nchini utasaidia kuongeza pato la taifa na kutoa
ajira kwa Watanzania.
Amesema Tanzania ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya
uwekezaji Tanzania Bara na Zanzibar hivyo ni wakati muafaka kwa
watendaji wa sekta husika kwa ushirikiano na serikali kujiimarisha
katika kuondoa ukiritimba ili kuvutia wawekezaji kutoka mataifa
mbalimbali Duniani.
Makamu wa Raia pia amefurahishwa na mpango wa wawekezaji
hao kutoka Korea Kusini ambao wanataka kusaidia uimarishaji wa haki za
wanawake hapa nchini na amekaribisha Jumuiya ya Wanawake kutoka Korea
Kusini kuja Kufanya ziara ya kikazi hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni