Jeshi
la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni
sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8
wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.
Akizungumza
na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo,
Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia
askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya
majambazi hao.
Amesema
baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi,
ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo
SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.
Akielezea
tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu
walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka
mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9
waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8
kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.
Amewataja
askari waliouawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo
Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC
Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.
Kufuatia
tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na wahalifu wote katika
maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza
oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na
kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.
"Mpaka
sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda
kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo
na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji…
mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani
ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu
tofati” amesema Marijani
Kuhusu
hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi
bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi
Katika
hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki
katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00
jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00
asubuhi hadi saa 12:00 jioni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni