Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi mshindi wa jumla Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa
Viwanda kwa mwaka 2016 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Devis
Deogratius (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa hafla ya utoaji waTuzo za Rais za Mzalishaji Bora
wa Viwanda kwa mwaka 2016 zilizofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za
Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)
kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora
nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji
bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba Serikali inatambua
mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo
ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.
Alisema mwaka wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni wa kazi
nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa
wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya
kukuza uchumi.
Alisema Serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda
kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa
umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa
kati.
Makamu wa Rais ambaye hotuba yake ilizungumzia mafanikio
na changamoto zinazokumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake,
amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na
imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa.
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumbua sekta ili serikali ifanye maamuzi.
Kwa sasa kuna Kamati inayoangalia namna bora ya
kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi chini ya Wizara ya
Viwanda , Bisahara na uwekezaji na inakaribia kumaliza kazi yake na
kuikabidhi Serikalini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni