Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,
leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe
za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika
Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama
lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania
kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea
kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja
atavunjika yeye.
''Muungano
ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein
tutaulinda Muungano kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja
atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.
Aidha
Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo
nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais
Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha
kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu
mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.
Aidha
amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana
mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe.
Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni
kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa
ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli na nchi
kavu.
Aidha
Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa
ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua
kwa demokrasia nchini.
Kwa
mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu
ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha
makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
''Niwahahakikishie
wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika
Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali
yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.
Sherehe
za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni
pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu
Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya
Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.
Kauli
mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya
muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na
Kufanya Kazi kwa Bidii''
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni