Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa
kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.
Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu
kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana
na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea
kufanyia majaribio makombora.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na
polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa
mchezo wa gofu.
Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju
China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari
kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la
nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.
THAAD ni nini?
- Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
- Hugonga kombora la kuliharibu
- Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
- Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni