Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata
utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo Jijini
Arusha,Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel
Daqarro.Picha na Vero Ignatus Blog.
Watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Meru wakiimba wimbo wa Taifa kama picha hapo juu inavyoonekana wakiongozwa na mwalimu Neema Lema ,na hii inayofuata hapa chini wakiongozwa na mtafsiri na mwalimu Viola Wilson .Picha na Vero Ignatus Blog
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha akiangalia kwa makini kile ambacho mtoto mwenye
ulemavu Amina kutoka shule ya msingi Meru akitumia kompyuta katika
kuhariri video aliyoichagua,aliyeshika kipazasauti ni mtaalam wa masomo
ya Tehama katika kitengo cha walemavu bi.Betha Denis.Picha na Vero
Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo amtembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa.
Akiwa
katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68 miongoni mwao wasichana
wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam
mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi
hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo.
Akisoma
risala mbele ya Mkuu huyo wa mkoa mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo
unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya
kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,384 wavulana wakiwa ni 709 na
wasichana wakiwa ni 675
Amesema
shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya Finland walioshirikiana na
Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili
wakichangia zaidi ya sh, milioni 180 huku fedha hiyo ikisaidia kujenga
jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop)
184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya
Laminationi na printa 4.
Pia
vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho
hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa
kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo
Gambo
alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa
wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa
elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi
Awali
Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa
kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veola Wilson na
Neema Lema
Gambo
anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi
mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James
uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua
kero zao
Gambo amewaagiza watumishi wa jiji la
Arusha wakiwemo wataalam wa vitengo mbalimbali kuhakikisha wanatatua
kero za wananchi haraka iwezekanavyo ili kuondokana na kero
zinazowakabili.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Visima viwili vya maji
vilivyoko magereza vilivyogharimu milioni 372, madarasa 6 Shule ya
msingi Olasity,madarasa 4 ya Shule ya msingi Burka Estate ambayo yamegaharimu jumla ya shilingi 218 milioni .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni