Kairuki amebainisha hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa uhakiki wa vyeti feki kwa Watumishi wa Umma lilioendeshwa na Serikali kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.
"Zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa kama Wabunge, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa sababu kwa mamlaka za uteuzi wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika tu...Watumishi 9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi sawa na asilimia 2.4 . Wenye vyeti vya utata ni 1,538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia 94...Hatua hazitachukuliwa kwa wenye vyeti feki tu, bali hata kwa wanaohusika kutengeneza vyeti hivyo". Alisema Kairuki
Aidha Mhe. Kairuki amewataka wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya kughushi waache mara moja kwa kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka saba.
Pamoja na hayo, Kairuki amepongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua kushughulika na zoezi hilo na kulimaliza kwa awamu moja tofauti na nchi nyingine zilichukua awamu tatu huku akitolea mfano wa kwa kuzitaja nchi hizo kwamba ni South Africa na Nigeria.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli amewaagiza Waziri Kairuki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaondoa watumishi wote waliobainika kuwa wanatumia vyeti vya kughushi 'hewa' huku akisisitiza kwamba yeye hawezi kuwasemehe watu walioghushi kwani wataondoka mara moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni