Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni
amesema viongozi waandamizi wa chama cha wananchi (CUF) ndiyo walihusika
na tukio la kulipua bomu katika nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu
Mhe. Masauni alieleza hayo Bungeni Jijini Dodoma jana pindi
alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Gandu kupitia
tiketi ya (CUF) visiwani Pemba, Mhe. Othuman Omary Hajji alipotaka kujua
kwanini mpaka leo hajizachukuliwa hatua stahiki kwa wafuasi wa CCM
waliochoma nyumba za wanachama wa CUF huko visiwani Tumbatu, huku akidai
serikali iliyopo madarakani siyo halali ni haramu kwa kuwa Jeshi la
Polisi lilichangia kumuweka madarakani Dkt. Ali Mohamed Shein.
"Ni kweli baada ya uchaguzi mkuu baadhi ya vyama vya
upinzani ikiwemo chake, viongozi walijitokeza kuhamasisha wananchi
kufanya mambo yanayokiuka sheria za nchi yetu.
"Kuna matukio mbalimbali yalijitokeza ikiwemo kuchomwa
moto nyumba, kuchoma mashamba, kurusha mabomu ikiwemo nyumba ya Kamishna
wa Jeshi la Polisi wa Zanzibar ambayo kwa uchunguzi uliofanyika mpaka
sasa, watu waliokamatwa kwa kuhusika urushaji bomu katika nyumba ya
Kamishna ni viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF)". Alisema Masauni
Pamoja na hayo, Masauni alisema Jeshi la Polisi
limeshakamilisha uchunguzi wake na jalada la mashtaka lipo kwa DPP muda
wowote kuanzia sasa litapandishwa Mahakamani ili sheria ichukuliwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni