Mwanamume
mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemfanyia
kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za makalio kwa
madai ya utoro shuleni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa
ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo Nuhu (14)
ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Igoma kwa
kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu
mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio,
tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25
Mei, 2017.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni.
Kamanda
Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili anaofanyiwa
mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa kuvumilia na
arehe 28 Mei.2017 aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi
Kamanda
Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upelelezi na mahojiano
na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani huku majeruhi akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na
hali yake inaendelea vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni