Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha 'The United Democratic Party' (UDP) ametangaza
rasmi kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kujipa fursa ya kuitumikia
familia yake.
Ole
Medeye ambaye alijiunga na UDP akitokea CHADEMA mapema mwaka jana,
ametoa kauli hiyo jana katika barua aliyomuandikia Mwenyekiti wa chama
hicho Mh. John Cheyo, huku akimshukuru kwa kumuani katika nafasi hiyo
kwa kipindi chote.
"Napenda
kukujulisha rasmi kwamba ili nipate muda wa kutosha kufanya shughuli za
ustawi na maendeleo ya familia na jamii inayonitegemea nimeamua kwa
hiari yangu kujiuzulu nafasi hiyo ya Katibu Mkuu kuanzia tarehe ya barua
hii".Imesema sehemu ya barua hiyo
Mwanasiasa
huyo amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Jimbo la
Arumeru Magharibi kupitia CCM katika Bunge la 10 na kupitia nafasi hiyo
aliweza pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
katika serikali ya awamu ya nne.
Mara
baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliamua kuhama chama na kujiunga na
CHADEMA ambapo hakudumu sana licha ya CHADEMA kumpa nafasi ya kugombea
nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha
alihamia UDP kabla ya kupewa nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni