Chama
cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri
Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto
mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa
shule ya Lucky Vicent
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael
Lekule ,alisema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya
wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi
,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.
Alisema
jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi
wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na
wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito
"Serikali
ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha familia 35 kwenda kupumzisha
wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia
inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na
serikali ya Magufuli," alisema Michael
"CCM
inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa
shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba
uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"alisema
Pia
alisema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye
mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20
ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje
kuiwakilisha serikali.
Hata
hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri
Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je
yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?
"Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," alisema Lekule
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni