Jeshi
la Polisi nchini limekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii zikiwahusisha askari wake kuwepo katika majina ya vyeti feki na
kusema taarifa hizo ni za uongo na wala hazijatolewa na Jeshi hilo.
Hayo
yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP
Advera Bulimba na kusema wanaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza taarifa
hiyo kwa lengo la kupotosha umma ili hatua kali za kisheria zichukuliwe
dhidi yake na kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
"Jeshi
la Polisi nchini, linaujulisha umma kwamba, orodha ya majina ambayo
yamekuwa yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakidai kuwa ni majina
ya askari wa jeshi la polisi wenye vyeti feki ni ya uongo na wala
taarifa hiyo haijatolewa na jeshi la polisi". Ilisema taarifa hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni