Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia
mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani
siku ya ajali iliyoua watu 35.
Akiomba
mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika
kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo
lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda.
Amesema
badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye
hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema
suala hilo halijatokea bungeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni