Majeruhi
wa ajali ya gari iliyohusisha vifo 35 vya wanafunzi, walimu pamoja na
dereva wa shule ya msingi Luck Vicent wilayani Karatu, wamesafirishwa
jana kwenda Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi .
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kia, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa majeruhi hao wanasafirishwa na ndege ya Shirika la Samaritan Purse ili kuwawezesha kupatiwa huduma za matibabu zaidi ambazo zitaweza kurejeshea afya zao.
Gambo
alisema kuwa Serikali imejitahidi kwa hali na mali kuhakikisha kuwa
wamewafariji wale wote waliofikwa na msiba na hata kuhakikisha kuwa
majeruhi waliobaki wanapatiwa huduma ambazo zitaweza kunusuru maisha
yao.
Gambo
aliwataka wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake kuacha kutumia
mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwa inakwamisha huduma za kijamii kwa
ajili ya kuchanganya na shuguli za kisiasa.
"Naombeni
sana wana Arusha muache kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwani hii
mitandao imepotosha sana mambo mengi imehusisha huduma za kijamii kuwa
mambo ya kisiasa hali ambayo inasababisha hata wanaojitokeza kuchangia
maafa haya kuvunjika moyo kwa ajili ya mambo yaliyoandikwa kwenye
mitandao ya hiyo"-alisema Gambo
Alidai
kuwa huduma za kijamii hazipaswi kuhusishwa na shughuli za kisiasa
kwani endapo zitahusishwa zitakwamisha hata wale wanaoendelea kufariji
kushindwa kuendelea na moyo huo.
Mbunge
wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye ni mmoja wa waliojitolea
kufanikisha safari hiyo aliwataka Watanzania kuendelea kuombea majeruhi
hao ili wapone haraka.
Safari
ya majeruhi hao kuelekea Marekani ilianza saa 5:40 asubuhi wakiambatana
na mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Gaspa ambaye amemwakilisha mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni