Mtangazaji
na Mchoraji katuni maarufu nchini Tanzania,Masoud Kipanya amewaaacha
watanzania midomo wazi kwa kuweka wazi maoni yake kuwa mwanaume hawezi
kuridhika na mwanamke mmoja.
Masoud
amesema tangia zamani wanaume ni Watu mwenye tamaa hivyo hakuna
mwanaume ambae anapenda kuwa na mwanamke mmoja ila ni vitu vidogo vidogo
tu vinavyozuia kama dini ya Kikristo na masuala mengine ya kiuchumi.
“Hakuna
mwanaume anaependa kuwa na mwanamke mmoja,na hiyo ndiyo huruka ya
uanaume,tunajizuia tu kwa sababu!! hivyo kwa mfano kwa wenzangu wakristo
utaratibu unawazuia lakini angalia vidumu vilivyo nje unaona eeehh??“Amesema Masoud Kipanya kwenye Mahojiano yake na Kwanza TV.
Hata
hivyo Masoud alizungumzia suala la idadi ya kuzaa watoto kwenye familia
na kusema kuwa kwa upande wake yeye hana kikomo kwenye kuzaa kwani
anaamini watoto hawarishwi na yeye bali wanarishwa na mwenyezi Mungu.
Masoud
Kipanya kwa mujibu wa Takwimu za mwaka jana zilizofanywa na kituo cha
Clouds FM kupitia kipindi cha XXl ni moja ya watu watatu maarufu nchini
Tanzania wanaoendesha magari ya kifahari akiwa anamiliki gari aina ya
Hummer H3.
==>Msikilize hapo chini akiongea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni