Tembo wakiwa wamejificha kwenye vichaka ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana.
Kwa
mujibu wa taarifa za Wahifadhi wa Wanyamapori inaelezwa kuwa sehemu ya
eneo hilo litakuwa ni njia ya tembo (maeneo ya mapito ya wanyamapori) ambayo
ilipitika kwa miaka mingi iliyopita na kwamba tembo wana kumbukumbu
hata kama walipita njia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Imeelezwa
kuwa njia hiyo ya mapito ya wanyamapori itakua ilitumiwa na wanyamapori
kuhama eneo moja hadi jengine ikiwemo maeneo ya hifadhi ya Taifa ya
Mikumi, Ruaha, Serengeti, Pori Tengefu la Rugwa na maeneo mengine ya
hifadhi na kwamba maeneo hayo mengi kwa miaka ya hivi karibuni
yameshaingiliwa na shughuli za kibinadamu ambazo hazisababishi tembo hao
kusahau njia hizo au kutokuzitumia tena.
Tembo
hao wakiwa ndani ya eneo chuo kikuu hicho cha Dodoma jana. Hakuna
madhara yeyote yaliyoripotiwa kusababishwa na tembo hao na taratibu za
kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi zimeshaanza kuchukuliwa na
uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Askari wa Wanyamapori
wameanza zoezi la kuwafukuza kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof.
Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa somo kwa wanafunzi wa
chuo kikuu cha Dodoma namna ya kuchukua tahadhari juu ya ugeni wa tembo
hao chuoni hapo.
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dodoma walikusanyika wakiwa na shauku ya kuwaona tembo hao.
Msafara
wa viongozi mbali mbali wa Serikali ukiambatana na Askari Polisi na
Askari wa Wanyamapori ukisogelea eneo walilokuwepo tembo hao kwa ajili
ya kuanza kuwafukuza kutoka katika maeneo hayo ya chuo kwenda kwenye
maeneo yao ya hifadhi.
Prof.
Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (wa pili kulia), Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete
(wa tatu kulia) na maafisa wengine wa Serikali na vyombo vya ulinzi na
usalama wakiangalia eneo walilokuwa wamejificha tembo hao chuoni hapo.
Askari
wa wanyamapori wakiingia ndani ya eneo walilokuwa wamejificha tembo hao
kwa ajili ya kuanza kuwafukuza eneo hilo kuelekea kwenye maeneo yao ya
hifadhi. Imeelezwa kuwa pindi tembo hao watakapofukuzwa kwa milio maalum
ya risasi hutafuta njia wanazozijua wenyewe za kurudi kwenye maeneo yao
ya hifadhi.
Tembo
hao wakianza kuondoka katika eneo hilo baada ya askari wa wanyamapori
kuanza kuwaondoa eneo hilo kwa kutumia milio maalum ya risasi.
(PICHA NA
HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni