Wabunge
wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema wa
Arusha Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa
uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jumatatu.
Jana
Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa miili ya wanafunzi 32, walimu
wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika
ajali ya gari.
Wa
kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa
fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa
salamu za rambirambi.
Lema
kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa
yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari
yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.
Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.
Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni