
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mhe Catherine Ruge ameanza
kutumikia uteuzi wake Bungeni kwa kuihoji serikali kuhusu mkakati wake
wa kuwekeza kwa usawa mkoani Mara.
Katika swali lake la nyongeza lililoelekezwa kwa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Mhe Ruge aliuliza, “Mkoa wa Mara una vivutio vingi
hasa kwa Eastern Corridor (ambao ni Upande ulio na Hifadhi ya
Serengeti) na Western Corridor (Upande ulio na Ziwa Victoria), lakini
serikali imewekeza zaidi kwa Eastern Corridor Upande wa Hifadhi kuliko
Western Corridor Upande wa Ziwa Victoria ambao ni kama umeshaulika, Je
ni nini mkakati wa serikali kuhusu Upande wa Ziwa Victoria na kwa
kuzingatia vivutio vingi vya asili vinapatikana ndani yake? Na Je
serikali INA mpango gani kuendeleza Upande wa Ziwa Victoria?”

Mbunge huyo pia kupitia ukurasa wake wa Facebook wa
Catherine Ruge alitoa wito kwa Watanzania wenye uzoefu na mazingira ya
ziwani na vyanzo kutoa mapendekezo na maoni yao ili kwa pamoja waweze
tambua namna ya kuwasilisha kwa Waziri wa Wizara husika.
“Niombe maoni yenu kwa watu mlio na uzoefu na mazingira ya
Ziwani na vyanzo vyake vya mapato ili kwa pamoja tushauriane niwe na cha
kusema baadae. Kwasababu Waziri wa Wizara husika ameniomba nionane nae
kwa maoni na mawazo niliyonayo kwa vyanzo vinavyopatikana Ziwani.
Ahsanteni sana. Karibuni” aliandika Mhe Ruge.
Ahsanteni sana. Karibuni” aliandika Mhe Ruge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni