Mbunge
wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe
amefunguka na kusema kuna matatizo makubwa katika manunuzi ya ndege aina
ya Boeing jambo ambalo limepelekea Mbunge huyo kuomba mkataba wa ndege
hiyo bungeni
Zitto
Kabwe amesema hayo baada ya gazeti la Jamhuri kuandika taarifa juu ya
ndege hiyo huku likisema kuwa Zitto Kabwe ameshindwa na kudai anapotosha
Umma juu ya taarifa za ndege hiyo, jambo ambalo Zitto Kabwe analipinga
vikali na kusema gazeti hilo linatumika na watu wanaohangaika kuficha
ukweli juu ya manunuzi ya ndege hiyo na kusema watake wasitake watajibu
tu ukweli.
"Nimeomba
mkataba wa ndege hii rasmi Bungeni. Nitawapa mrejesho. Kuna tatizo
kubwa kwenye manunuzi haya. Boeing Airplanes wamepaniki sana na
wanunuzi, wamekazana kuficha ukweli kuhusu ununuzi wa Ndege hii.
Watajibiwa tu, aste aste" alisema Zitto Kabwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni