Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya
wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent
ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani
Karatu Mkoani Arusha.
Na Vero Ignatus, Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mama
Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi wa Arusha kuiaga miili ya
wanafunzi 32 , Walimu 2 na Dareva 1 wa shule ya Lucky Vincent ya Arusha
ambao waliofariki katika ajali ya gari tarehe 6 mei 2017 saa tatu
asubuhi katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Katika shughuli hiyo ya kuiaga miili hiyo ambayo
imehudhuriwa viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi amesema kuwa
ipo sababu ya jeshi la polisi wazazi pamoja na waalimu kuzingatia
usalama barabarani.
Hata hivyo amemshukuru Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa
kuguswa na msiba huu ambapo amemtuma waziri wa elimu kutoka nchini Fred
Matiang'i kuja kushiriki katika msiba huo mzito wa Kitaifa.
Amesema kuwa msiba huu siyo wa taifa la Tanzania peke yake
bali ni msiba wa Afrika kwa ujumla ambapo amesema pigo hili linatufanya
kufanya marekebisho ya matendo yetu.
Ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuwa waadilifu
wawapo barabarani kubeba abiria kulingana na uwezo wa gari,wametakiwa
kukumbuka kuwa serikali inapiga vita vilevi , madawa ya kulevya pamoja
na mwendo kasi.
Amelitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani
wafuatilie na kuhakikishekuwa alama za barabarani zipo sawa ,pia kuweka
vibao mahali panapotakiwa kwani
Msiba huu umetupa majonzi mengi watanzani na kila mtu. Aidha amewataka wamiliki wa shule pamoja na waalimu kuhakikisha kuwa magari ya shule yanachukua abiria kwa uwezo unaotakiwa kwani haipendezi kila mara kusikia taifa linakubwa na misiba.
Msiba huu umetupa majonzi mengi watanzani na kila mtu. Aidha amewataka wamiliki wa shule pamoja na waalimu kuhakikisha kuwa magari ya shule yanachukua abiria kwa uwezo unaotakiwa kwani haipendezi kila mara kusikia taifa linakubwa na misiba.
Ikumbukwe kuwa ajali hii iliyosababisha vifo vya wanafunzi
32 walimu 2 na dereva 1 ilisababishwa na gari aina ya T 871 BYS coaster
rosa kuacha njia na kudumbukia korongoni, ambapo mashuhuda wa ajali
wanadai "ni Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na dereva kutokuwa mzoefu na
njia hiyo",ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumamosi 6 Mei 2017 majira ya
saa tatu asubuhi katika mteremko wa mlima Marera kata ya Rhotia, wilaya
ya Karatu Mkoani Arusha.
Katibu
Mkuu wa CCM , Komredi Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya
wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na
Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa
ajali ya gari wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Elimu wa Tanzania , Prof. Joyce Ndalichako akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Elimu wa Tanzania , Prof. Joyce Ndalichako akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Elimu wa Kenya, Mhe. Fred Matiang'i akiwahutubia na kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Mwakilishi kutoka Zanzibar , akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto, Bi. Ummy Mwalimu akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha
waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya
Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe
06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Boniface Mhuya akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango akiwahutubia maelfu ya
wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na
Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa
ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Askofu Josephat Lebulu akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Prof. Joyce Ndalichako akiongozana na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu akielekea kutoa heshima za mwisho kwa wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Mbunge wa Arusha Mhe. Godbless Lema na Mkewe wakiongozana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kwenda kutoa heshima zao za mwisho wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha. Picha Zote na Gadiola Emanuel.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni