Na,Vero Ignatus,Arusha
Kutokana na mvua
inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha
imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa
sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote
watano.
Mkasa huo wa
kusikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na
maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.
Kamanda wa
polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili
wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini
Arusha.
Mkumbo
aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio
alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili
wa shule ya sekondari ya Inaboishu.
Kamanda
alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia
Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru
Mkoani Arusha.
Amesema
watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo
aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki (26) na Best
Jonathani(20).
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia
nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji
la Arusha na Mkoa kwa ujumla.
Alisema na kuitakia
pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake
kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu
mgumu kwake.
Kamanda
Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika
kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na
kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.
Amesema
kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine
hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.
Aidha
kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa
jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na
kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari
hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni